BUNDA.
Mwanaume mmoja, Mukoba Juma mkazi wa Kijiji cha Guta B wilayani Bunda mkoani Mara ameshambuliwa na kuuawa na Kiboko katika ufukwe wa Ziwa Victoria wakati akifanya shughuli za uvuvi.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Guta B, Kisheri Nyihande amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa juzi saa 12 jioni marehemu pamoja na rafiki yake aliyemtambulisha kwa jina moja la Madege walienda kuvua katika ziwa Victoria kwa lengo la kupata kitoweo.
Nyihande alisema wakiwa katika shughuli hiyo ghafla alijitokeza mnyama huyo na aliyemrusha marehemu ndani ya maji huku yeye Madege akitimua mbio kunusuru maisha yake.
Alifafanua kuwa Madege alipiga kelele kitendo kilichowafanya wananchi kufika katika eneo la tukio na kuanza kuutafuta mwili wa marehemu ambao hata hivyo ulipatikana jana saa tatu asubuhi ukiwa na majeraha makubwa na mwili huo kuzikwa jana saa 10 jioni

No comments:
Post a Comment