Tuesday, 4 March 2014

UBOVU WA MITARO KITUO CHA MABASI MWENGE NI KEROO JIONEE

 Hii ni sehemu ya maduka ambayo kwa mbele ya hayo maduka maji yamejaa kutokana na kuziba kwa mitaro ya eneo la stendi ya daladala ya Mwenge jijini Dar es salaam
 Sehemu hii kuna mtaro wa maji lakini kutokana na kuziba kwake imekuwa kero kwa wafanyabiashara na watu wanaotumia stendi ya Mwenge kwani mitaro hiyo imeziba na kupelekea maji kujaa na kuingia barabarani hata madukani.
 Maji ya mvua yakiingia kwenye mtaro wa maji ambao kwa mbele kumezibwa kutokana na uchafu ulioko kwenye mtaro huo wa stendi ya Mwenge
 Hii ni sehemu ya mtaro mmojawapo ambao unapokea maji mengi pale mvua inaponyesha lakini hayawezi kwenda kwani pameziba.
 Eneo hili ndipo daladala zinapoingilia kwenye kituo cha Mwenge kilichopo Kinondoni. Eneo hili halipitiki wakati wa mvua ikinyesha kutokana na mitaro mingi kuziba na kujaa maji  mengi ndani ya stendi hii.
 Sehemu hii pameja maji lakini kwa chini kuna mtaro mkubwa ila kutokana na kuziba inapelekea maji kujaa sehemu kubwa ya maduka na hata barabarani.
 Unaweza kusema ni mto lakini kumbe ni maji ya mvua yaliyotuhama kutokana na mitaro kuziba
 Hii ndio hali halisi kama inavyoonekana katika picha
 Kutokana na kuziba kwa mitaro hiyo maji yanaingia mpaka kwenye barabara ya Bagamoyo inayopita karibu na kituo hicho cha Mwenge.

No comments: