Je unatumia bidhaa kama mikanda, mabegi, viatu na wakati mwingine nguo
zinazotumia ngozi ya nyoka, leo nakuletea picha hapa uone jinsi nyoka
wanavyouawa na kuchunwa ngozi ili wewe upendeze.
Kuna njia mbalimbali zinazotumika kuua na kuchuna ngozi ya nyoka huko
Indonesia. Lakini njia ambayo ni ukatili ambapo nyoka wanauawa na
kuchunwa ngozi kwaajili ya kutengeneza mikoba haswa na kuuzwa nchi za
Magharibi kwa zaidi ya shilingi milioni 6.5 (pauni za Uingereza 2400).
Pamoja
na gharama yote hiyo huko Ulaya na Marekani, mkoba huo unapatikana kwa
sawa na shilingi za Kitanzania 54,000(pauni 20) nchini Indonesia kwenye
soko la ngozi ya nyoka ambapo nguo na vipuri mbalimbali huuzwa.
Moja ya machinjio ya nyoka yalionesha jinsi nyoka wanavyovuliwa ngozi
yao ni kijiji kimoja kijulikanacho kama Cirebon, nchini Indonesia.
Ukiangalia katika picha hizi utaona jinsi wafanyakazi wanavyoua na
kuchuna ngozi nyoka zaidi ya elfu kwa wiki.
Katika maeneo hayo bei ya mkoba uliotengenezwa kwa ngozi ya nyoka
unaweza kuwa kati ya shilingi 24,000(pauni9) mpaka 48,000 kutegemea na
ukubwa. Ngozi ya nyoka inapofika nchi za Magharibi katika nyumba za
mitindo bei hupanda maradufu mpaka awa na shilingi milioni 6.5
ANGALIA ZAIDI...
No comments:
Post a Comment