Rais Vladimir Putin wa Urusi, amesema bado hakuna haja kwa nchi yake kupeleka majeshi nchini Ukraine.
Bwana Putin amesema Urusi ina haki ya kutumia njia zote kulinda raia wake walioko mashariki mwa Ukraine.
Amekanusha
taarifa kwamba majeshi ya Urusi yamewazingira raia wa Ukraine walioko
katika jimbo la Crimea, bali ni watu wanaoiunga mkono Urusi na ambao
wanajilinda wenyewe.
Bwana
Putin amesema kuondolewa madarakani kwa Rais Viktor Yanukovych katika
mji mkuu wa Ukraine, Kiev ni "ukiukaji wa katiba na uporaji wa madaraka
kijeshi.".
Amesema
wapiganaji hao wameitumbukiza Ukraine katika "vurugu". Pia amesema
wapigania utaifa na wapinga usemiti wanarandaranda katika mitaa ya Kiev
na miji mingine.
Amesema iwapo watu wanaozungumza Kirusi mashariki mwa Ukraine watahitaji msaada wa Urusi, basi Urusi itakubaliana na ombi lao.
"kama tutaona hali hii ikianza kutokea maeneo ya mashariki, tuna haki ya kutumia kila njia" amesema.
Bwana
Putini amesema katika jimbo la Crimea watu wenye silaha wanaoiunga mkono
Urusi na raia wamezingira kambi za kijeshi za Ukraine, sio askari wa
Urusi.
"Majeshi ya eneo hilo kwa ajili ya kujilinda" ndiyo yanayohusika na kuchukuliwa kwa majengo ya serikali katika Crimea, amesema.
Uhasama
umeongezeka katika kituo cha kijeshi cha Belbek karibu na Sevastopol,
mji wa bandari ambao ni kambi ya majeshi ya majini ya Urusi.
Akizungumzia
kupinduliwa kwa Bwana Yanukovych, Bwana Putin amesema kiongozi huyo
aliyeondolewa madarakani nchini Ukraine alikubali matakwa yote ya
wapinzani.
Bwana Putin amesisitiza kuwa Bwana Yanukovych bado ni rais halali wa Ukraine.
Amesema kuna mambo matatu ya kumwondoa madarakani rais, ameyataja kuwa ni kifo, kujiuzulu au kushtakiwa.
Bwana
Yanukovych alikimbilia Urusi, na Bwana Putin aliwaambia waandishi wa
habari: "Sifikiri kama ana mustakabhali mwema kisiasa".
Urusi ilimsaidia kwa sababu za "kibinadamu", amesema, "vinginevyo angekuwa ameuawa"
No comments:
Post a Comment