Thursday, 6 March 2014

UN-ICTR Yatoa Msaada wa Magari ya Kiusalama kwa Polisi Arusha

Bwana Robert Foot akikabidhi funguo za magari hayo kwa Kamanda Sabas

 Kamanda Sabas akitoa shukrani zake kwa uongozi wa UN-ICTR kwa msaada huo. Katikati ni Afisa Habari wa Mahakama hiyo Bw. Danford Mpumilwa 

Mahakama ya Umoja wa Mataifa inyoshughulikia Mauaji ya Halaiki ya Rwanda (UN-ICTR) iliyo na makao yake makuu mjini Arusha leo imetoa msaada wa magari mawili ya kiusalama (Amoured Cars) kwa jeshi la polisi mkoani Arusha ili kuimarisha shughuli zake za kiusalama mkoani hapo. Magari hayo ni baadhi ya yale yliyokuwa yakitumika kwa shughuli za usalama  - kubebea watuhumiwa au watu nyeti - na mahakama hiyo inyotarajiwa kumalisha shughuli zake mwakani. Magari hayo ni yale yaliyoimarishwa kiusalama ambapo hata risasi haziwezi kupenya kwenye bodi yake au kwenye kioo chake. Magari hayo yalikabidhiwa na Mkuu wa Idara ya Fedha na Kaimu Mkuu wa Utawala wa Mahakama hiyo Bw. Robert Foot kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo Afande Liberatus Sabas

No comments: