Mmiliki wa facebook, mtandao wa kijamii mkubwa kuliko yote
duniani, Mark Zuckerberg akiwa katika mkakati wa kutimiza lengo lake la
kuunganisha dunia, sasa anadaiwa kufikiria kutumia ndege zisizokuwa na rubani
kusambaza huduma hiyo ili kutimiza ndoto yake.
Kwa mujibu wa TechCrunch, mmiliki wa mtandao huo, anadaiwa
kuwa katika maongezi ili kununua Titan Aerospace (PICHANI KUSHOTO), hii ni kampuni inayozalisha
ndege (drone) ambazo hazina rubani na zinatumia jua kama chanzo cha nishati
yake.
Ndege hizo zinazojulikana kama “atmospheric satelltees”
zinaweza kutumika kusambaza mawasiliano, na kufikisha sauti pamoja na huduma ya
data kwa maili nyingi kwani ziko katika njia ya mzunguka wa dunia.
Facebook wanafikiri wangependa kutumia huduma hiyo kusambaza
mawasiliano katika maeneo ambaya hayana mtandao na si rahisi kufikisha
mtandao. Kampuni hiyo ina mpango wa kuanza kupeleka ndege hizo
zisizokuwa na rubani katika bara la Afrika na kwamba watatengeneza ndege
11,000
kwa kuanzia, kwa mujibu wa TechCrunch.
Ununuzi huo utakuwa ni maendeleo makubwa ya internet, ambayo
ni jitihada na mchango mkubwa wa Facebook na baadhi ya makampuni ya simu za
mikononi ambapo yataleta na kutoa fursa kwa watu zaidi ya bilioni 5 duniani
ambao kwa sasa hawana.
Drone hizo za Titan zinaweza pia kuisaidia vizuri Facebook
ambayo imejitanua zaidi kwa kununua mtandao wa kijamii wa Whatsapp ambao
ulinunuliwa hivi karibuni kwa dola za kimarekani bilioni 19 ambao ni maarufu
sana katika nchi zinazoendelea ili kupata zaidi huduma ya internet.
Facebook ndio utakuwa mtandao wa kwanza kujaribu huduma hiyo
ya ndege ambazo hazina rubani, mwaka jana Google walianziasha Project Loon,
mradi mdogo ambao unatumia nishati ya jua kufikisha internet katika maeneo
yasiyofikika.
No comments:
Post a Comment