Butiama.
Mtu mmoja ameuawa na wananchi kwa kukatwa katwa na
mapanga baada ya kuwavamia askari polisi katika kituo cha polisi cha
Butiama mkoani Mara.
Kaimu Kamanda wa polisi mkoani Mara Paulo
Kasabago amethibitisha kutokea kwa tukio hilo jana saa 9 alasiri ambapo
imedaiwa kuwa marehemu huyo alifika katika kituo hicho na kuchomoa panga
uliokuwa ndani ya mkoba mgongoni mwake na kuanza kuwashambulia askari
polisi walikuokuwepo kituoni hapo.
Kasabago aliwataja askari waliokatwa mapanga kwenye tukio hilo kuwa ni
Grantha namba WP.9533 PC aliyekatwa sehemu ya mikononi na mguu wa
kulia pamoja na askari mwingine Israel namba F.8901 D/C aliyekatwa
kifuani baada ya kutoka ndani ya kituo kuja kutoa msaada kwa Grantha.
Kasabago alisema baada ya askari hao kupiga
kelele mtu huyo alianza kukimbia ambapo wananchi waliokuwa jirani
walimkimbiza kwa kumshambulia kwa mawe, fimbo na mapanga
kilichosababisha kifo chake akiwa anapatiwa matibabu kwenye hospitali
ya wilaya ya Butiama.
Katika tukio lingine mwanaume mmoja ameuawa kwa vipigo na kuchomwa moto katika Kijiji cha Kabasa Tarafa ya Serengeti wilayani Bunda baada ya kudaiwa kuiba mbuzi watatu mali ya Saasita Sekule(49).
Alisema wananchi hao baada ya kumuua mtu huyo walichoma nyumba tano moto na kuziteketeza mali ya Mazwanja Lwangumba ambaye alituhumiwa kuwa mwanae Butiku Mazwanja alishirikiana na marehemu katika wizi wa mbuzi hao.
Kasabago alisema katika tukio hilo watu wawili ambao ni Saasita Sekule na na Alfred Mtogwa wana shikiliwa jeshi la polisi kwa kutuhumiwa kuhusika katika tykio hilo.
No comments:
Post a Comment