Sheikh Issa Bin Shaaban Simba. |
Mufti wa Tanzania, Sheikh Issa Bin Shaaban Simba ameondoka nchini kuelekea India kwa ajili ya matibabu.
Aliongozana
na ujumbe wa watu wawili, akiwemo Katibu Mkuu wa Baraza la WaislamU
Tanzania(BAKWATA), Suleiman Lolila na Diwani wa Kata ya Kwadelo wilayani
Kondoa, Omari Kaliati.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyomfikia mwandishi na kuthibitishwa na Naibu
Katibu Mkuu wa Bakwata anayeshughulikia Utawala, Yusufu Yasini, Sheikh
Simba aliondoka saa 10 jioni kwa kutumia ndege ya Shirika la Oman Air.
Mufti
alifika uwanjani hapo na kuingia kupitia eneo la wageni mashuhuri (VIP)
huku akisindikizwa na msafara wa pikipiki ya polisi.
Naibu
Katibu Mkuu wa Bakwata anayeshughulikia Dini, Mohammed Khamis aliahidi
kutoa taarifa zaidi kwa mwandishi, kuhusiana na safari hiyo.
Mara
baada ya kutapa taarifa za safari hiyo juzi, mwandishi alimtafuta Naibu
Katibu Mkuu Utawala wa Bakwata, aliyekiri Mufti kusafiri.
"Sipo
katika nafasi nzuri ya kuzungumzia suala hilo kwa kuwa nipo barabarani,
naendesha gari, nitafute kesho (jana) nitaweza kukupa taarifa vizuri,"
alisema Yusufu.
Alipotafutwa tena jana kupitia simu yake ya mkononi, hakuweza kupatikana baada ya simu hiyo kuwa imezimwa.
Juhudi
za kuwatafuta viongozi hao zinaendelea kufanywa na mwandishi ili kupata
taarifa zaidi ya safari ya kiongozi huyo mkuu wa Waislam nchin
No comments:
Post a Comment