“PRESS RELEASE” TAREHE 20.03.2014.
- MTOTO WA MIAKA 07 AFARIKI DUNIA BAADA YA KUPIGWA NA BABA YAKE MZAZI.
- MTU MMOJA AUAWA BAADA YA KUPIGWA NA KUNDI LA WANANCHI KWA TUHUMA ZA WIZI
- MTEMBEA KWA MIGUU AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI KATIKA AJALI YA BARABARANI.
- JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA RAIA WA KIGENI WATANO KWA KOSA LA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTOTO
AITWAYE IREENE MARCO MBEMBELA (07) MWANAFUNZI CHEKECHEA SHULE YA MSINGI
MIGOMBANI NA MKAZI WA SOGEA ALIFARIKI DUNIA WAKATI AKIENDELEA KUPATIWA
MATIBABU KATIKA KITUO CHA AFYA TUNDUMA.
MAREHEMU
ALIPIGWA KWA KUTUMIA FIMBO SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE HADI
KUPOTEZA FAHAMU NA BABA YAKE MZAZI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MARCO
MBEMBELA (30) MKAZI WA SOGEA – TUNDUMA.
TUKIO
HILO LILITOKEA TAREHE 19.03.2014 ALFAJIRI HUKO SOGEA KATA NA TARAFA YA
TUNDUMA WILAYA YA MOMBA KWA TUHUMA KUWA ANATABIA YA KUZURURA OVYO
KATIKA NYUMBA ZA WATU.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z.
MSANGI ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI KUTUMIA BUSARA KATIKA KUWAELEKEZA
NA KUWAONYA WATOTO WAO BADALA YA KUWAPIGA KWANI NI HATARI KWA AFYA NA
MAISHA YAO.
PIA HUKO WILAYA YA KYELA:
MTU
MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MATESO LAMSI (25) MKAZI WA KIJIJI CHA
NDOBO ALIUAWA KWA KUPIGWA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA KUNDI LA
WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI WAKITUMIA SILAHA ZA JADI
FIMBO, MAWE NA MARUNGU.
TUKIO
HILO LILITOKEA TAREHE 18.03.2014 SAA 20:00 USIKU KATIKA KIJIJI CHA
NDOBO, KATA YA NDOBO, TARAFA YA NTEMBELA, WILAYA YA KYELA. CHANZO CHA
TUKIO HILO NI TUHUMA ZA WIZI BAADA YA MAREHEMU KUKAMATWA AKIIBA KAKAO
KWENYE SHAMBA LA JAPHET MWAKALINGA.
MAREHEMU
ALIKUWA MHALIFU MZOEFU NA AMETOKA GEREZANI HIVI KARIBUNI. KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z.
MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI
KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE WAWAFIKISHE WATUHUMIWA WANAO
WAKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI KATIKA MAMLAKA HUSIKA KWA HATUA ZAIDI ZA
KISHERIA.
AIDHA KATIKA TUKIO JINGINE:
MTU
MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA GODFREY KAYANGE (22) FUNDI MAGARI, MKAZI
WA MAKAMBAKO ALIFARIKI DUNIA MUDA MFUPI WAKATI ANAPATIWA MATIBABU
KATIKA HOSPITALI YA WILAYA MBARALI BAADA YA KUGONGWA NA GARI LENYE
NAMBA ZA USAJILI T.859 AGL/T.650 AKB AINA YA SCANIA TRUCK LILILOKUWA
LIKIENDESHWA NA DEREVA BENJAMIN MANDELE (38) MKAZI WA MAFINGA.
AJALI
HIYO ILITOKEA TAREHE 19.03.2014 SAA 16:00 JIONI KATIKA KIJIJI CHA
MKOMBE, KATA YA UBARUKU, TARAFA YA RUJEWA, WILAYA YA MBARALI MKOA WA
MBEYA KATIKA BARABARA YA MBEYA/NJOMBE.
CHANZO
CHA AJALI NI UZEMBE WA DEREVA KUTOKUMUONA MAREHEMU WAKATI AKIDANDIA
GARI HILO NA KUMGONGA. MTUHUMIWA AMEKAMATWA NA GARI LIPO KITUO CHA
POLISI RUJEWA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z.
MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO
HASA KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA
AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA ENEO LA KASUMULU:
JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA RAIA WA PAKISTAN WATANO AMBAO NI
1. MOHAMED RASHID (35), 2. SADAM HUSSEIN (19), 3. NAWICED IGBILI (23),
4. GULU LAZA (31) NA 5. MUZZAFAR HAMED (24) WOTE WAKAZI WA NCHINI
PAKISTAN WAKIWA WAMEINGIA NCHINI BILA KIBALI.
WAHAMIAJI
HAO HARAMU WALIKAMTWA TAREHE 18.03.2014 SAA 18:00 JIONI HUKO KATIKA
ENEO LA KASUMULU, KATA YA NGANA, TARAFA YA UNYAKYUSA WILAYA YA KYELA.
WATUHUMIWA WAMEKABIDHIWA IDARA YA UHAMIAJI.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z.
MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUTOA TAARIFA ZA WATU WANAOWATILIA MASHAKA
KATIKA MAENEO YAO ILI UCHUNGUZI ZAIDI UFANYWE DHIDI YAO.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.