Friday, 10 October 2014

Mgonjwa aliefariki kwa Ebola Marekani

Screen Shot 2014-10-10 at 8.38.50 AMFamilia ya mgonjwa wa kwanza wa Ebola aliefia nchini Marekani imelalamika kwamba kama ndugu yao angepewa uangalizi na matibabu kama inavyotakiwa basi asingepoteza uhai wake.
Thomas Duncan alietokea Afrika Magharibi zaidi ya siku 18 zilizopita ambapo mchumba wake aitwae Louise Troh waliekua waoane baada ya Duncan kuwasili Marekani, ni mmoja wa watu wa karibu waliolalamikia huduma mbovu na ‘kubaguliwa’ kwa Duncan baada ya kugundulika kuwa mgonjwa wa Ebola hivyo anataka uchunguzi ufanywe.
Anasema Duncan alipotua Texas kwa mara ya kwanza aliambiwa aende nyumbani na wala hakupimwa kama anavyo virusi vya ugonjwa wa Ebola pamoja na kwamba aliwaambia Manesi kwamba ametokea Liberia ambako kuna Ebola.
Screen Shot 2014-10-10 at 8.38.05 AM
Reverend Jesse Jackson akiwa na mama mzazi wa Duncan.
Ndugu mwingine wa kiume wa Duncan amesema mgonjwa wao hakuwa chini ya uangalizi mzuri kama ilivyotakiwa na alibaguliwa kwa sababu ya weusi wake, yani kuna wale Wagonjwa wazungu waliokutwa na Ebola waliwekewa uangalizi mzuri mpaka wakapona ila huyu sababu ni mweusi akatelekezwa.
Screen Shot 2014-10-10 at 8.37.39 AM
Hii picha ni Duncan akiwa na ndugu yake muda mfupi baada ya kuwasili Marekani kwenda kumuoa mchumba wake wa siku nyingi.
Screen Shot 2014-10-10 at 8.37.19 AM
Louise Troh mchumba wa Marehemu Duncan anaeonekana upande wa kulia.
Duncan aliekua na umri wa miaka 42 muda mfupi kabla ya kufariki alikua akitaka kumuona mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka 19 anaeonekana kwenye picha hapa chini lakini haikuwezekana.
Screen Shot 2014-10-10 at 8.54.47 AM
Hawa kwenye picha hapa chini ni watu waliobobea kwenye usafishaji na waliitwa kufanya usafi kwenye nyumba aliyokua anakaa Duncan huko Dallas Texas kabla ya kwenda Hospitali ambapo vitu vyake kama mashuka na mataulo vilibaki kwenye nyumba hiyo kwa siku tano baada ya yeye kupelekwa Hospitali.
Screen Shot 2014-10-10 at 8.56.18 AM

No comments: