Eneo
la Shule ya Msingi Magamba ambalo linadaiwa kuuzwa kwa wakandarasi
wanaotengeneza barabara ya Sitalike –Mpanda kwa Kiwango cha lami
likichimbwa kifusi.
Kibao Shule ya Msingi Magamba Halmashauri ya Nsimbo
(Picha na Kibada kibada –Nsimbo Mlele)
Na Kibada Ernest Kibada Mpanda Katavi
SEHEMU ya eneo
la Shule ya Msingi Magamba Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo , Mlele Mkoa
wa Katavi limeuzwa kwa wakandarasi wanaotengeneza barabara kwa kiwango
cha Lami kutoka Sitalike hadi Mpanda Mjini .
Eneo hilo la shule limeuzwa kwa Mkandarasi wa Kampuni ya Kichina lijulikanayo kwa Jina la Railway Sevanth Group lenye Makao yake jijini Dar es salaam.
Eneo hilo limenunuliwa kwa ajili ya kuchimba kifusi kinachotumika kutengenezea barabara ya lami inayoendelea kujengwa kutoka Kata ya Sitalike hadi Mpanda Mjini.
Akizungumzia kuhusu eneo hilo kuuzwa
kwa Mkandarasi huyo Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Magamba Mwl. Yohana
Kasansa ameeleza kuwa yeye hatambui kuuzwa kwa eneo hilo bali
anatakumbua kuwani eneo halali la Shule.
Akaeleza kuwa yeye anaona tu
shughuli zikiendelea za uchimbaji wa kifusi kwa ajili ya kutengeneza
barabara lakini hajui nani alitoa ruhusa.
Alisema eneo hilo la shule hutumika kwa ajili ya kulima mazao aina ya mahindi kwa ajili chakula cha shule kwa watoto.
Mwalimu Kasansa akaongeza kuwa wakati
linapokuwa halitumiki kwa ajili ya kilimo huwa linaachwa wazi lakini
baada ya kuchimbwa udongo kwa ajili ya kifusi limebaki na mashimo ambayo
ni hatari kwa watoto na hasa wakati huu ambao mvua zinapokaribia
kunyesha.
Naye Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Magamba George Pius alipotakiwa kuelezea uuzwaji wa eneo la Shule ambayo ni mali ya Kijiji, alisema kuwa hatambui ni nani aliuuza.
“Kufuatia hali hiyo niliwaandikia
barua ya kuwataka wasitishe shughuli za kuchimba kifusi katika eneo hilo
ili kupata ufumbuzi wa suala hilo lakini hawakutekeleza na waliendelea
na kazi kama unavyoona hapo kazi zikiendelea”alisema Pius Afisa Mtendaji
wa Kijiji cha Magamba.
No comments:
Post a Comment