Wednesday, 8 October 2014

Coastal Union kuiburuza Mahakamani Kampunni ya Binslum Tyre

Na Mwandishi Wetu, Tanga
UONGOZI wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga umesema utakwenda mahakamani kuishitaki Kampuni ya Binsul Tyre kutokana na kitendo cha kutengeneza tisheti za Coastal Union zenye nembo ya kampuni Sound na kuwapa bure mashabiki kuingia nazo kwenye mechi mbalimbali za ligi kuu Tanzania bara wakiwa wamelipiwa na viingilo vya mchezo husika.
Hali hiyo ni kinyume na utaratibu kutokana na kuwa tayari kampuni hiyo ilishajitoa kufadhili timu hiyo na tayari klabu ya Coastal Union ilikwishapata mfadhili mwingine ambayo ni kiwanda cha Kutengeneza Unga Ngano mkoani Tanga cha Pembe Flours Mills.
Kauli hiyo imetolewa kwenye kikao cha Kamati ya Utendaji Kilichoketi mwishoni mwa wiki ambapo kilikuwa na agenda nne za msingi ambazo ni Suala la mshambuliaji wa Coastal Union Danny Lyanga,Utoaji slipi benki,Jezi za Sound,Tarehe ya Uchaguzi.
Kikao hicho kilihudhuriwa na viongozi wa mbalimbali akiwemo Mwenyekiti wa Klabu ya Coastal Union,Steven Mguto,Katibu Mkuu Kassim El Siagi,Mjumbe wa Kamati ya Utendaji,Albert Peter Saimu Amiri na Meneja wa Coastal Union Akida Machai.
Kama unavyojua kuwa Kampuni ya Binslum Tyres ilikuwa mhisani wetu na sasa hatuko naye na tayari alishapeleka fedha zake kwenye vilabu vingine ikiwemo Mbeya City sasa tunamshangaa kuendelea kufanya biashara ya matangazo kupitia mashabiki wetu kwa kuwapa tisheti za kuvaa bure ikiwemo kuwalipia viingilio kwenye mechi za ligi kuu zinazochezwa Mkwakwani.
Hivyo kutokana na suala hilo tayari uongozi wa Coastal Union umeshamkamata mshabiki mmoja ambaye ni wakala wa kusambaza tisheti hizo kwa mashabiki na kumpeleka polisi na taratibu za kisheria zinaendelea ili kuweza kukomesha vitendo hivyo ambavyo sio vya kiungwana.
Tayari Kampuni ya Pembe Flours Mills ilishasaini mkataba na Klabu ya Coastal Union wa kuifadhili timu ya Coastal Union kwa kipindi cha mwaka mmoja ambapo tayari makubaliano hayo yameshaanza kutekelezwa
 
Hata hiyo kikao hicho kilipendekeza tarehe ya kufanyika uchaguzi mdogo wa kama ilivyo maagizo ya shirikisho la soka nchini (TFF) kuitaka kufanya uchaguzi wa kujaza nafasi zilizokuwa wazi kwenye safu ya uongozi wa Klabu hiyo.
Kamati hiyo imependekeza kuwa uchaguzi huo ufanyika Novemba 23 mwaka huu mkoani Tanga.
Ambapo kimsingi uchaguzi huo unafanyika ili kuweza kuziba nafasi zilizokuwa wazi ambayo ni Mwenyekiti na wajumbe wawili wa kamati ya utendaji.
Hata hiyo alisema kuwa wanatarajia kuunda kamati ya uchaguzi ambayo itasimamia uchaguzi huo ili kuweza kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika

No comments: