Na Mwandishi wetu
MADEREVA
wa Kampuni ya Usafiri Dar es Salaam (UDA), wanaofanya safari kati ya
Mnazimmoja na Kivukoni jana waligoma kufanya kazi wakipinga agizo la
uongozi kuwataka wapeleke hesabu ya sh 300,000 kwa siku.
Kutokana
na mgomo huo abiria wanaosafiri katika njia hiyo, walipata usumbufu
hadi pale ufumbuzi wa mgogoro huo ulipopatikana majira ya saa moja
asubuhi.
Akizungumza
niaba ya madereva na makondakta jijini Dar es Salaam, mmoja wa
madereva, ambaye hakupenda jina lake liandikwe kwenye mtandao huu wa eddy blog,
alisema, wamekuwa wakifanya kazi katika manyanyaso makubwa kuhusu
hesabu.
Alisema
sababu zilizowafanya wagome zimetokana na ukweli kwamba kutokana na
ushindani wamagari katika njia hiyo, wanauhakika fedha hizo haziwezi
kupatikana kirahisi.
“Sisi
tunaulaumu uongozi wa kampuni hii kwani umekuwa ukiendeshwa kikabila na
mabavu, pindi wafanyakazi tunapo hoji haki zetu za msingi,”alisema
dereva hyo.
Alisema
baada ya uongozi kupata taarifa kuwa wamegoma, alifikia mmoja wa
viongozi katika eneo la Mmnazimmoja ambako walikuwepo madreva hao na
kuwashawishi waanze kazi kwa kutumia hesabu ya awali ambayo ni sh
205,000.
Hata
hivyo kiongozi huyo, aliwashangaza madereva hao pale alipowaambia kuwa
wataanza kukusanya hesabu hiyo y ash 300,000 baada ya kuzisimamisha
kampuni nyingine zinazotoa huduma hiyo katika njia hiyo.
“Unajua
watu wakituona hivi wanajua tunalipwa vizuri kumbe wala sio hivyo kwa
mfano makondakta wote hawakuajiriwa, tulioajiriwa ni sisi madereva ambao
hata mshahara wenyewe hatuupati kwa wakati huku tukitakiwa kununua sare
za kazi na kupeleka sh 5000 ya kuoshea gari kila siku,”alisema.
Aliongeza
kuwa viongozi wa kampuni hiyo wamekuwa mara kwa wakitoa lugha za
vitisho za kumfukuza kazi kila mfanyakazi anayepingana na maamuzi ya
uongozi hata kama unakandamiza haki zao.
Akizungumzia
kuhusu ajira katika kampuni hiyo, alisema kwa kuwa kiongozi mkuu wa
kampuni hiyo anatoka Kanda ya Ziwa, hivyo nafasi nyingi za ajira
zimekuwa zikienda kwa kabila la wasukuma.
Alipotafutwa
msemaji wa UDA, George Maziku, kuyatolea ufafanuzi malalamiko hayo,
alisema madereva wote waliojaribu kugoma wamewaondoa na kuwapeleka njia
nyingine kauli ambayo imetofautiana na madereva.
Akisema madereva waliopelekwa baada ya kuondolewa hao waliopinga wamekubali kupeleka hesabu y ash 300,000.
“Kuhusu
suala la ukabila huyo dereva aliyesema hivyo ni mpumbavu kama yeye siyo
msukuma ungemuuliza ameingiaje, na hili la kuondolewa kampuni nyingine
katika njia hii, hili halina ukweli wowote,”alisema Maziku.
No comments:
Post a Comment