TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 08.10.2014.
- MTU MMOJA AFARIKI DUNIA NA WENGINE KUJERUHIWA BAADA YA MAGARI MAWILI KUGONGANA.
- JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA RAIA NA MKAZI WA WA NCHINI ETHIOPIA KWA KOSA LA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA
MAKAZI YAKE, UMRI ATI YA MIAKA 25 – 30 AMEFARIKI DUNIA WAKATI AKIWA
ANAPATIWA MATIBABU BAADA YA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.397 AQT AINA
YA ISUZU LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE NOEL MAHENGE
KUGONGANA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.505 BYG/T.843 CUG AINA YA
SCANIA LIKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE GODFREY PHILIMON (37) MKAZI WA
TUKUYU WILAYA YA RUNGWE.
AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE
07.10.2014 MAJIRA YA SAA 09:45 ASUBUHI HUKO CHAPWA, KATA NA TARAFA YA
TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA YA
MBEYA/TUNDUMA.
AIDHA, KATIKA AJALI HIYO WATU
WAWILI WALIJERUHIWA NA KULAZWA KATIKA HOSPITALI YA SERIKALI TUNDUMA
AMBAO NI 1. SHABANI KIPANDE (22) MKAZI WA UYOLE NA 2. MUDDY MSELEMU
(25). CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI WA GARI T.397 AQT AINA YA ISUZU.
DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA AJALI NA JITIHADA ZA KUMTAFUTA
ZINAENDELEA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA SERIKALI
VWAWA – MBOZI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA
KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI
ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA, ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA
MAHALI ALIPO DEREVA ALIYEKIMBIA KUZITOA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI
AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
TAARIFA ZA MISAKO:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
LINAMSHIKILIA RAIA NA MKAZI WA NCHINI ETHIOPIA AITWAYE SEYIM LATABO (45)
KWA KOSA LA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.
MHAMIAJI HUYO ALIKAMATWA MNAMO
TAREHE 07.10.2014 MAJIRA YA SAA 07:50 ASUBUHI HUKO KATIKA STENDI YA
MABASI – TUKUYU, KATA YA KAWETELE, TARAFA YA TUKUYU MJINI, WILAYA YA
RUNGWE, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA AMESHAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA HATUA
ZAIDI ZA KISHERIA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
WAGENI KUFUATA TARATIBU ZA KUINGIA NCHINI ILI KUEPUKA MATATIZO NA
MADHARA YANAYOWEZA TOKEA.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
No comments:
Post a Comment