NIPASHE
Mwenyekiti wa BAWACHA Halima Mdee na wenzake nane jana walikosa dhamana na kupelekwa rumande katika gereza la Segerea hadi leo maombi ya dhamana yatakaposikilizwa tena.
Mdee pamoja na wenzake nane walifikishwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka mawili likiwemo la kutotii amri halali ya Jeshi la Polisi na kufanya mkusanyiko usio halali.
Baada ya kusomewa mashtaka na Hakimu Janeth Kaluyenda washktakiwa waliyakana makosa yote na upande wa mashtaka ulidai kuwa upepelezi wa kesi hiyo umekamilika.
Hakimu alisema dhamana ipo wazi kwa kila mmoja asaini bondi ya shilingi Milioni1 na kuleta wadhamini wawili ambao mmoja kati yao anafanya kazi katika taasisi inayotambulika kisheria lakini iliahirishwa hadi leo itakaposomwa tena baada ya mawakili kupinga.
MWANANCHI:
Mgogoro mwingine mkubwa wa kifamilia wa kugombea maiti umeibuka mjini Moshi na kusababisha mwili wa Rosemary Marandu kuhifadhiwa mochwari kwa siku34.
Mwili wa marehemu huyo aliyefariki dunia Septemba4 umehifadhiwa katika hospitali ya KCMC na umekua ukilipiwa shilingi 9,000 kila siku hivyo siku34 gharama yake ni sh306,000.
Mama mzazi wa marehemu alisema mumewe aitwaye Flavian Marandu ndiye anayeshikilia mwili huo hadi sasa bila kutoa sababu yoyote kutokana na kushindwa kuelewana na familia yake.
Hata hivyo baba wa marehemu alisema habari hizo si za kweli na kwamba mkewe anamzushia uongo kwani ameshindwa kuja kupanga taratibu za mazishi.
MWANANCHI
3.Shindano la Miss Tanzania 2014 ambalo lilikua lifanyike jumamosi halitafanyika tena hadi pale kesi ya msingi iliyozua mzozo baina ya wakurugenzi wa Lino Agency wanaoratibu mashindano hayo itakapomalizika.
Mahakama ya Kisutu ilitupa pingamizi la muda lililowasilishwa na Hashimu Lundenga akipinga maombi ya zuio la muda la kusimamishwa kwa mashindano hayo lililowasilishwa na mshirika wake Prashant Patel.
Katika uamuzi wake Hakimu Frank Moshi alikubaliana na hoja za wakili wa wa Patel,Benjamini Mwagamba kwamba mahakama yake ina mamlaka ya kusikiliza maombi ya zuio na kwamba yameletwa chini ya vifungu vinavyostahili.
HABARILEO
Rais Jakaya Kikwete amesema kuna ushahidi wa baadhi ya mabalozi hapa nchini wanaoziwakilisha nchi zao kujihusisha na siasa hali inayohatarisha amani ya nchi
Kadhalika amesema wamekua wakichanganya siasa na dini kwa kutumia dini kuunga mkono baadhi ya vyama vya siasa na shughuli za kisiasa kwa ujumla.
Amewaasa wananchi kutojiingiza katika siasa na wasiingize siasa katika dini na badala yake waiokoe nchi katika majanga makubwa yanayoweza kutokea kutokana na kutumia dini kuendeleza siasa.
MTANZANIA
Utafiti uliofanywa na Chama cha waandishi wa habari wanawake nchini TAMWA umeonyesha asilimia 55.5 ya wanaume katika Wilaya ya Kinondon ni walevi na kusababisha kukithiri kwa vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia.
Msimamizi wa utafiti huo Dk Severine Kessy alisema kwa upande wa kinamama ulevi upo kwa asilimia40 wakati asilimia60 hawatumii kabisa kilevi.
Alisema pamoja na mambo yote asilimia63 ya waliohojiwa ambao ni watumiaji wa pombe kila siku walisema nyumba zao ziko chini ya hatua100 kutoka sehemu ambazo pombe zinauzwa.
TANZANIADAIMA
Mkazi wa Mtwara Elias Edward amefariki dunia baada ya kupigwa na mchi kichwani katika ugomvi wa kulishwa nyama ya paka.
Kamanda wa polisi Mtwara alisema marehemu aliuawa na mwanae Said Lukas ambaye ndiye aliyepika kitoweo hicho na kumpa baba na mama yake ambao hawakujua ilikua ni aina gani ya nyama.
Inasemekana mtuhumiwa huyo alikuta paka huyo ameuawa na watoto waliokua wanacheza kisha kumchukua na kwenda nae nyumbani ambapo alimchemsha vizuri na kuwatengea wazazi wake.
Baada ya kugundua ni paka ulizuka ugomvi mkubwa kati yao na baadae mtuhumiwa kumvizia na kumpiga kichwani hadi kufa.
UHURU
Wauguzi wa Hospitali ya Bugando wakiendelEa kuchangisha gedha kwa ajili ya kupatikana lishe kwa watoto mapacha watatu ambao wamempoteza mama yao,shangazi wa watoto hao ametoroka na fedha za misaada zilizotolewa na wasamaria wema.
Mapacha hao walizaliwa katika hospitali ya Misungwi wakiwa ni watoto watatu walionusurika kati ya watano waliozaliwa ambapo mama yao alifariki muda mfupi baada ya kujifungua pamoja na watoto wengine wawili.
Kutokana na tukio hilo wauguzi wamesitisha kuomba misaada kupitia namba ya simu iliyotolewa badala yake wafike hospitali na kuikabishi kwa bibi anaewalea.
Zaidi ya shilingi laki mbili zilichangwa kupitia simu hiyo lakini hazikuweka kutumika baada ya shangazi yao huyo kutoweka nazo akidai anakwenda kuzitoa kwa wakala.
MWANANCHI
8.Rais wa Zanzibar Mohamed Shein amemtimua kazi mwanasheria mkuu wa Zanzibar Othman Masoud baada ya kukataa ibara22 za katiba iliyopendekezwa wakati wa bunge maalum la Katiba mjini Dodoma.
Taarifa iliyotolewa kwenye vyombo mbalimbali vya habari ilisema Shein amempandisha cheo aliyekua naibu Mwanasheria mkuu Said Hassan kushika nafasi hiyo.
Othmani alionekana kuwaudhi baadhi ya wajumbe ndani ya bunge hilo na kumzoea baada ya kuahirishwa bunge aliondoka kwa kupitia mlango wa nyuma wa ukumbi wa bunge hilo chini ya ulinzi mkali.
Hata hivyo alisema licha ya kuwa yeye ni Mwanasheria alitumia utashi wake wa kidemokrasia kupiga kura kuzikataa ibara hizo kutokana na kutoridhishwa na jinsi zilivyoandikwa

No comments:
Post a Comment