Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Dkt. Rehema Nchimbi akihutubia wakati wa dua ya kuiombea Katiba mpya Inayopendekezwa
Viongozi wa Dini toka wadhehebu ya
Kiislamu, Kikristo, Wasabato, Wahamadiya, Jamaat Khan, Singh Temple
pamoja na CCT-Dodoma wakiongoza dua zao leo mjini Dodoma.
(Picha zote na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma)
Na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma.
DUA ya shukurani ya kuiombea
Katiba mpya Inayopendekezwa imefanyika jana mjini Dodoma na viongozi
mbalimbali wa dini toka madhehebu mbalimbai yakiwemo ya Kiislamu,
Kikristo, Wasabato, Wahamadiya, Jamaat Khan, Singh Temple na CCT-Dodoma.
Akiongea wakati wa dua hiyo,
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi, Mhe. Dkt.
Rehema Nchimbi alisema kuwa katika mchakato mzima wa kusaka katiba mpya,
shughuli mbaoimbali za maendeleo zikiwemo shughuli za kibiashara,
shughuli za kibenki, wanafunzi na shughuli nyingine za kiofisi ziliweza
kuendelea kama kawaida pasipo shari yoyote hadimchakato wa kuipata
Katiba ulipofikia.
Dkt. Nchimbi alieleza kuwa, kuna
watu waliotumia muda wao mwingi katika kuhakikisha kuwa mchakato
unafikia lengo kwa kukesha usiku na kufanya dua maalum ya kuiombea
katiba hiyo ili iweze kupatikana na aliongeza kuwa wapo waliofanya kazi
kubwa kwa kukesha huku wakifanya kazi ndani ya Bunge Maalum kwa ajili ya
kufanikisha mchakato huo.
“Kipindi hiki cha mchakato wa
Katiba, Watanzania na marafiki zetu tumeongea na Mungu kwa namna isiyo
ya kawaida, tumekutana hapa kukiri kwa maana tulimuita Mungu naye
ametuitikia, hakika yeye ndiye aliyetufanya kuipata Katiba hii”,
alisema Mhe. Nchimbi.
Nao Viongozi wa dini mbalimbali
walipata wasaa wa kutoa dua zao kwa Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kuiombea
nchi amani pamoja na Katiba yenyewe kwani itakuwa mkombozi kwa
Watanzania.
Akiongea kwa niaba ya Baraza la
Wazee wa Dodoma, Mhe. Balozi Job Lusinde alisema kuwa ni jambo la busara
kuomba dua kwa Mungu kuhusu mchakato wa kupata Katiba na pia ni wasaa
wa kumshukuru Mungu kwa kuwawezesha wale wote waliojitolea kufanikisha
kuipata Katiba hiyo.
Aidha, alisema kuwa tangu Dkt.
Nchimbi awe Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, watu wameshuhudia msimamo wake
kuhusu umuhimu wa umoja, upendo, mshikamano kwa wananchi wote wa Dodoma
kwani ameweza kuzishirikisha dini zote, na kuwaunganisha, pia amekuwa wa
kwanza katika kuutukuza mji wa huo wa Dodoma.
“Ndugu zangu wananchi wa Dodoma,
tumshukuru RC wetu wa Dodoma, Dkt. Rehema Nchimbi pamoja na Kamati yake
ya Ulinzi na Usalama kwa kutupa muda wa dua kama hii ya leo”, alisema
Balozi Lusinde.
No comments:
Post a Comment