Friday, 10 October 2014

kutana na hii Tshirt ya maneno ya Kiswahili aliyovaa Seneta wa Nairobi ikiwatusi ‘wazungu’

UH 4
UH 2Mike Sonko ni yule Mwanasiasa mwenye vituko ambae alipata umaarufu sana toka akiwa mbunge kwa kuwa na swagg zake kivyakevyake, alikua mbunge kijana ambae anaingia na hereni bungeni, blingbling kibao kama cheni na pete kama anavyoonekana ametupia kwenye hii picha hapa juu akiwa sasa ni Seneta wa jiji la Nairobi.
Sasa juzi kati Rais Uhuru Kenyatta alikwenda The Hague Uholanzi kwenye Mahakama ya ICC kwa hiyo Wakenya wenzake wanaopinga huo uamuzi wa ICC na kuona ni usumbufu wakajilipia nauli zao ili kwenda kumsupport ambapo Seneta huyu ni mmoja wa waliojilipia na kulipia wengine pia.
Pamoja na Sonko kwenda huko akiwa na dukuduku la kukerwa na maamuzi ya Mahakama hiyo akiitaka imuache Rais wao wa Kenya afanye kazi, aliamua kuvaa tshirt yenye maandishi ya Kiswahili ‘ikiwatusi’ Wazungu kama anavyoonekana kwenye hii picha hapa chini.
Kwenye hizi picha hapa chini anaonekana Seneta wa jiji la Nairobi Mike Sonko na Tshirt ambayo alianza kuivaa toka akiwa Airport Kenya kwenda Uholanzi yenye maneno yanayosomeka >>>mumheshimu Rais wetu takataka nyinyi gasia
Sonko 2Kwenye picha nyingine Sonko anaonekana akiwa amewasili mahakamani ICC na kikosi chake kisha wakafanya maandamano mafupi kabla ya kumpa support Rais Uhuru kwa kuimba wimbo wa taifa na nyimbo za kizalendo wakati kesi ya Uhuru ikiwa inaendelea Mahakamani.
Tayari Rais Uhuru Kenyatta amerejea Kenya jana asubuhi na kupokewa na maelfu ya Wakenya ambao hawakupendezwa na kilichofanywa na Mahakama hiyo.
Muda mfupi tu baada ya kuwasili jana Rais Kenyatta alipiga vijembe Mahakama hiyo kwa kusema ‘Walikua wanafikiria kwamba tutakataa kwenda mi nikawaambiwa ile kitu itakataa kuja huko ni Urais wa Wakenya, tumeenda tumekaa huko masaa matatu hatujaambiwa chochote… hatukufungua mdomo sasa hata nashindwa kujua nilikwenda kufanya nini
Ile kitu hawajafahamu kwa vichwa vyao ni kwamba kama nchi ya Kenya tumetoka safari ndefu, na wasifikiri ya kwamba hatujui ni mahali gani tulifanya makosa, sisi tunawaambia hapana….. tuko na suluhu ya shida zetu‘ – Uhuru
Uh 1

UH 3

No comments: