Saturday, 25 October 2014

Hii ya noti ya shilingi elfu moja Tanzania umeipata

Shillingi elfu 1
Kumbukumbu zako ziko sawa kuhusu yale malalamiko ya kukosewa kwa picha ya baba wa taifa hayati Mwalimu Nyerere kwenye noti ya shilingi elfu moja? basi kama hazipo sawa, ichukue hiyo.
Baada ya hayo malalamiko unaambiwa Benki Kuu ya Tanzania imesema imeanza kufanyia kazi malalamiko ya kukosewa kwa picha ya Rais wa kwanza wa Tanzania, Marehemu Mwalimu Julius Nyerere ambapo mkurugenzi wa huduma za kibenki Emmanuel Boaz amesema tayari benki hiyo imeanza kufanyia kazi hayo malalamiko baada ya kusoma katika mitandao ya jamii.
Mwananchi wameandika mkurugenzi huyo alisema BoT haijapata taarifa rasmi kutoka kwa mtu yoyote lakini wameamua kuzifanyia kazi taarifa hizo >>>“Na sisi tumesoma katika mitandao, hakuna taarifa rasmi tuliyoipata lakini hatuwezi kudharau tuhuma hizo na endapo tukigundua kuna matatizo tutachukua hatua za kubadilisha haraka”
Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, suala la picha kukosewa sio geni kwani ilishawahi kutokea mara kadhaa kwa marais wastaafu na BoT ililazimika kubadili haraka ili kutoharibu mtazamo wa Taifa ambapo alitoa mfano wa picha ya Mwalimu Nyerere kukosewa na kuonekana nguo aliyovaa imefanana na blauzi lakini pia picha ya Rais Ally Hassani Mwinyi ambayo ilionekana shingoni ana mikunjo.
Kutokana na hali hiyo, mkurugenzi huyo aliwatoa hofu Watanzania kuwa endapo itabainika kama noti hizo zina kasoro zitarekebishwa ambapo hivi karibuni, mitandao ya kijamii iliwakariri wanafamilia ya Rais huyo wa kwanza wakilalamikia picha hiyo kwenye noti ya Sh1,000 kukosew

Friday, 10 October 2014

MADEREVA WA MABASI YA UDA WAGOMA, ABIRIA WALAZIMIKA KUTEMBEA KWA MIGUU.

Na Mwandishi wetu
MADEREVA wa Kampuni ya Usafiri Dar es Salaam (UDA), wanaofanya safari kati ya Mnazimmoja na Kivukoni jana waligoma kufanya kazi wakipinga agizo la uongozi kuwataka wapeleke hesabu ya sh 300,000 kwa siku.
Kutokana na mgomo huo abiria wanaosafiri katika njia hiyo, walipata usumbufu hadi pale ufumbuzi wa mgogoro huo ulipopatikana majira ya saa moja asubuhi.
Akizungumza niaba ya madereva na makondakta jijini Dar es Salaam, mmoja wa madereva, ambaye hakupenda jina lake liandikwe kwenye mtandao huu wa eddy blog, alisema, wamekuwa wakifanya kazi katika manyanyaso makubwa kuhusu hesabu.
Alisema sababu zilizowafanya wagome zimetokana na ukweli kwamba kutokana na ushindani wamagari katika njia hiyo, wanauhakika fedha hizo haziwezi kupatikana kirahisi.
“Sisi tunaulaumu uongozi wa kampuni hii kwani umekuwa ukiendeshwa kikabila na mabavu, pindi wafanyakazi tunapo hoji haki zetu za msingi,”alisema dereva hyo.
Alisema baada ya uongozi kupata taarifa kuwa wamegoma, alifikia mmoja wa viongozi katika eneo la Mmnazimmoja ambako walikuwepo madreva hao na kuwashawishi waanze kazi kwa kutumia hesabu ya awali ambayo ni sh 205,000.
Hata hivyo kiongozi huyo, aliwashangaza madereva hao pale alipowaambia kuwa wataanza kukusanya hesabu hiyo y ash 300,000 baada ya kuzisimamisha kampuni nyingine zinazotoa huduma hiyo katika njia hiyo.
“Unajua watu wakituona hivi wanajua tunalipwa vizuri kumbe wala sio hivyo kwa mfano makondakta wote hawakuajiriwa, tulioajiriwa ni sisi madereva ambao hata mshahara wenyewe hatuupati kwa wakati huku tukitakiwa kununua sare za kazi na kupeleka sh 5000 ya kuoshea gari kila siku,”alisema.
Aliongeza kuwa viongozi wa kampuni hiyo wamekuwa mara kwa wakitoa lugha za vitisho za kumfukuza kazi kila mfanyakazi anayepingana na maamuzi ya uongozi hata kama unakandamiza haki zao.
Akizungumzia kuhusu ajira katika kampuni hiyo, alisema kwa kuwa kiongozi mkuu wa kampuni hiyo anatoka Kanda ya Ziwa, hivyo nafasi nyingi za ajira zimekuwa zikienda kwa kabila la wasukuma.
Alipotafutwa msemaji wa UDA, George Maziku, kuyatolea ufafanuzi malalamiko hayo, alisema madereva wote waliojaribu kugoma wamewaondoa na kuwapeleka njia nyingine kauli ambayo imetofautiana na madereva.
Akisema madereva waliopelekwa baada ya kuondolewa hao waliopinga wamekubali kupeleka hesabu y ash 300,000.
“Kuhusu suala la ukabila huyo dereva aliyesema hivyo ni mpumbavu kama yeye siyo msukuma ungemuuliza ameingiaje, na hili la kuondolewa kampuni nyingine katika njia hii, hili halina ukweli wowote,”alisema Maziku.

WANANCHI WASALIMISHA BUNDUKI MBILI AINA YA SMG KWA JESHI LA POLISI



 


kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Lineratus Sabas akionyesha moja ya silaha ambazo zimesalimishwa  na wananchi
Jeshi la polisi mkoani Arusha limefanikiwa  kupata silaha mbili aina ya SMG ambazo  zilisalimishwa na wananchi katika siku mbili tofauti  huko wilayani ngorongoro.


Akiongea na waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoani Arusha Lineratus Sabas  alisema kuwa Silaha hizo zilisalimishwa na wananchi katika siku tofa uti tofauti ambapo alisema kuwa silaha ya kwanza ilisalimishwa September 19   silaha aina ya SMG yenye NO.563651071iliopatikana katika eneo la harash ikiwa na risasi  mbili ndani ya magazine .
Alibainisha kuwa silaha ingine  ilisalimishwa September 26  ikiwa ni aina ya SMG yenye namba  ya usajili 514142 hii ilipatika katika eneo  hilo hilo la harash wilayani  Ngorongoro


Aliwapongeza wanachi kwa kutii sheria ya kusalimisha silaha hiiuku akitoa wito kwa wananachi wote popote pale walipo kusalimisha silaha ambazo wanahisi wanazitumia kinyume cha sheria.

Aidha alisema kuwa kama kuna mwananchi yeyote anaisi kuwa anamali nyingi na anaitaji kumiliki silaha basi afuate sheria zinazotakiw

LORI LA KAMPUNI YA COCA COLA LILIVYOPATA AJALI LUGALO JIJINI DAR

 Kioo cha lori cha  mbele kikiwa kimepasuka.
 Makreti ya soda yalivyoanguka.
 Baadhi ya kreti za soda zikiwa zimezagaa eneo la ajali.Mmoja wa wahusika akitoka kuzima na kuuchomoa ufunguo wa gari lililopata ajali.
 Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) akilinda usalama eneo hilo.
 Watu wakishuhudia ajali hiyo.
  Chupa zikiwa zimeanguka kwenye mtaro.
Sehemu ya foleni inayosababishwa na gari hilo.

WATU watatu akiwemo dereva wa gari la kampuni ya soda ya Coca Cola walipata michubuko kadhaa katika ajali iliyotokea leo asubuhi maeneo ya Lugalo, jijini Dar es Salaam.
 
Akizungumza na mtandao huu,  mmoja wa mashuhuda amesema chanzo cha ajali hiyo ni baada ya gari ndogo kuingia ghafla mbele ya gari hilo  kubwa lililokuwa limebeba vinywaji na  ndipo gari kubwa likiwa katika kukwepa likajikuta likianguka ubavu

MWALIMU AZICHAPA NA MWANAFUNZI WAKE LIVE DARASANI KISA BANGI

Mwalimu wa sayansi katika shule ya Santa Monica High School alimstukia mwanafunzi huyu akijaribu kuuzia wanafunzi wenzake bangi darasani. 

Alipomkabili kuhusu tendo hilo, mwanafunzi huyo alimsukuma mwalimu huyo na ghafla ngumi zikaanza kurushwa hewani.



Mwanafunzi huyo, Blair Moore, alikamatwa na polisi na kufunguliwa mashitaka ya kuingiza madawa, na kisu shuleni.

blair moore Mwalimu na mwanafunzi wapigana darasani. Wanafunzi warekodi video badala ya kuamulia
Mwanafunzi huyo, Blair Moore, akiwa chini ya ulinzi wa polisi
Mwalimu huyo, Mark Black, ambaye pia ni kocha wa mieleka shuleni hapo, alisimamishwa pamoja na malipo kwa muda wakati uchunguzi wa tukio unaendelea; si kama adhabu, bali ni utaratibu wa shule za jimbo hilo.



Wanafunzi wengi walijitokeza kum-support mwalimu huyo, kwa kusema alijihami baada ya kushambuliwa kwanza. Walianzisha mpaka Facebook Page, “We Support Coach Black of Samohi” ambayo imepata zaidi ya Likes 20,000. “Samohi” ni kifupi cha Santa Monica High [school]




Mwalimu huyo aliruhusiwa kurudi kazini baada ya uchunguzi kuonyesha hakuwa na hatia
coach black Mwalimu na mwanafunzi wapigana darasani. Wanafunzi warekodi video badala ya kuamulia

Wanafunzi wengi walikuwa upande wa mwalimu huyo

WATU 7 WALIOUAWA KWA UCHAWI KIGOMA NA NYUMBA 18 KUCHOMWA MOTO

Moja ya nyumba zilizoteketezwa katika Kijiji cha Murufiti ambapo watu saba waliuawa kwa kuchomwa moto. Picha na Diana Rubanguka. 

Watu saba wameuawa kwa kuchomwa moto ndani ya nyumba katika tukio ambalo nyumba 18 ziliteketezwa na mbili kubomolewa na wananchi waliodai wanawaua wachawi katika Kijiji cha Murufiti, Kasulu, mkoani Kigoma.
Polisi wameeleza kuwa tayari watu 17 wamekamatwa kwa kuhusika kwenye tukio hilo.
Miongoni mwa waliouawa katika tukio hilo lililotokea Jumatatu iliyopita ni John Mavumba (68) na mkewe Elizabeth Kaje 55 ambao pamoja na wenzao walikuwa wakituhumiwa kuwa ni washirikina.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Josephat John ambaye ni mtoto wa Mavumba, alisema wazazi wake walichomwa moto na kundi la vijana waliokuwa wakiwatuhumu kuwa ni wachawi.
Alisema vijana walikuwa wamebeba mapanga, marungu na kupita katika nyumba mbalimbali wakifanya mauaji wakisema maneno kwa kurudiarudia kwamba watawamaliza wachawi kwa kuwaua, ndipo yeye na wenzake walikimbia usiku huo wakihofia kuuawa.
“Niliporudi alfajiri niliukuta mwili wa mama ukiwa umbali wa mita 10 kutoka ilipo nyumba yetu ukiwa umeungua na mwili wa baba ukiwa umeungua ndani ya nyumba,” alisema John.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Jafari Mohamed alisema mauaji hayo yalitokea Oktoba 6 kuanzia saa 4:00 usiku katika kijiji hicho.
John alisema baada ya tukio hilo wanaume wengi wameyakimbia makazi yao wakihofia kuuawa na kundi la vijana hao. “Kijiji kimebaki na wanawake tu, wanaume wamezikimbia nyumba zao wanahofia kuuawa,” alisema.
Mohamed alisema mauaji hayo yametokana na imani za kishirikina.
Aliwataja waliouawa kuwa ni John Muvumba (68), Elizabeth Kaje (55), Dyaba Kitwe (55), Vincent Ntiyaba (42), Herman Ndabiloye (78), Redempta Mdogo (60) na Ramadhan Kalaliza (70) wote wakazi wa kijiji hicho.
Alisema nyumba zilizochomwa moto ni 18, mbili zilibomolewa na kufanya jumla ya nyumba 20 zilizoharibika kabisa.
Wakazi wa kijiji hicho, Zablon Andrew na Eveline Enock walisema kwa nyakati tofauti kuwa chanzo cha mauaji hayo ni mganga wa jadi aliyefika kijijini hapo na kupiga ramli akiwataja watu waliouawa kuwa ni wachawi.
Andrew alisema baada ya mganga huyo kuwataja, vijana walikusanyana na kuanza kuwateketeza watu bila huruma.
“Kitendo hiki kimeturudisha nyuma kimaendeleo kwa sababu nyumba zetu zimechomwa moto na mazao yetu yameharibiwa,” alisema Andrew.
Hali ilivyo kijijini
Mmoja wa watu aliyechomewa nyumba, Evelyne Msilu alisema sasa kijiji hicho kina askari wengi wanaofanya doria.
“Hali inasikitisha, tumepoteza ndugu zetu waliouawa, wanaume wengi wamekikimbia kijiji kwa hofu ya kuuawa na vijana wengine wamekimbia wakiogopa kukamatwa,” alisema.
Kwa nini ipigwe ramli?
Akisimulia, Enock alisema kuna kijana mmoja katika kijiji hicho ambaye kazi yake ni kufyatua matofali aliwaomba vijana wanzake kuwa siku inayofuata wamsaidie kuyapanga katika tanuru.
Alisema jambo la ajabu ni kwamba walipoamka asubuhi walikuta matofali yamekwishapangwa na haikujulikana aliyefanya kazi hiyo.
Alisema kijana huyo na wenzake waliamini kwamba waliofanya kazi hiyo ni wachawi.
Akisimulia kisa kingine, Enock alisema siku chache zilizopita kuna msiba ulitokea kijijini hapo na baada ya mazishi, siku iliyofuata walikuta msalaba umeng’olewa na haujulikani ulipo, jambo ambalo pia lilihusishwa na ushirikina.
Ofisa mtendaji wa kijiji hicho, Ogen Gasper aliyeomba Serikali kujenga kituo cha polisi kijijini hapo, alisema baada ya kupata taarifa za tukio hilo alifanya jitihada kubwa kuwapata askari, lakini hawakufika kwa kilichodaiwa ni kukosa usafiri.
Gasper alisema hilo ni tukio la tatu kwa watu kuuawa kwa kutuhumiwa kuwa ni wachawi, la kwanza likiwa limetokea mwaka 1996.
via>>Mwananchi

MAGAZETI YOTE YA LEO IJUMAA TAREHE 10.10.2014




31_b9422.jpg
26_b47b5.jpg


1_e3da8.jpg
2_cdb71.jpg30_efd2b.jpg
3_eb937.jpg
4_a4242.jpg27_762ed.jpg
5_1ee15.jpg29_1b5b6.jpg
6_52c7e.jpg28_57920.jpg
32_67184.jpg
8_5d7ce.jpg
33_93975.jpg
34_c20d0.jpg

MAGAZETI YA UDAKU LEO OKTOBA 10,2014





Uliiona hii picha ya Polisi wa Tanzania iliyosambaa mitandaoni? hatimaye maamuzi yametangazwa

Kama kila siku huwa unaingia facebook, whatsapp au instagram inawezekana ukawa ulikutana na hii picha ya Askari Polisi ambao walipigwa picha wakiwa wanakiss wakiwa ndani ya sare za jeshi hilo.
Sasa taarifa mpya iliyotoka baada ya hii picha kuzidi kusambaa ni kwamba Jeshi la Polisi Kagera limechukua maamuzi ya kuwafukuza kazi askari hawa wawili pamoja na mwingine mmoja ambae ndio aliipiga hii picha kupitia simu yake ya mkononi.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Henry Mwaibambe amewataja askari hao kuwa ni PC Asuma Mpaji Mwasumbi mwenye namba F.7788,PC Fadhili Linga mwenye namba G 2122 na PC Veronica Nazaremo Mdeme na wote walikuwa askari wa kikosi cha usalama barabarani wilayani Missenyi.
ASKARIKamanda Mwaibambe amezungumza na ITV na kusema askari hao walitenda kosa hilo la fedhea kwa kupiga picha kinyume na maadili ya jeshi hilo mwaka 2012 wakiwa kazini na kwamba PC Fadhili ndiye aliyehusika na kupiga picha hizo kwa kutumia simu yake ya mkononi na kuituma katika mitandao mbalimbali ya kijamii kitendo ambacho ni kinyume cha maadili kwa sababu mbalimbali.
Mwaibambe amekiri kuwa picha husika inayoonekana kwenye mitandao ni picha halisi ambayo haijachakachuliwa hivyo ni wazi kila askari kujua maadili ya kijeshi yapo kisheria na askari yeyote anafundishwa namna ya kuishi katika maisha ya utumishi wa jeshi la Polis

Mgonjwa aliefariki kwa Ebola Marekani

Screen Shot 2014-10-10 at 8.38.50 AMFamilia ya mgonjwa wa kwanza wa Ebola aliefia nchini Marekani imelalamika kwamba kama ndugu yao angepewa uangalizi na matibabu kama inavyotakiwa basi asingepoteza uhai wake.
Thomas Duncan alietokea Afrika Magharibi zaidi ya siku 18 zilizopita ambapo mchumba wake aitwae Louise Troh waliekua waoane baada ya Duncan kuwasili Marekani, ni mmoja wa watu wa karibu waliolalamikia huduma mbovu na ‘kubaguliwa’ kwa Duncan baada ya kugundulika kuwa mgonjwa wa Ebola hivyo anataka uchunguzi ufanywe.
Anasema Duncan alipotua Texas kwa mara ya kwanza aliambiwa aende nyumbani na wala hakupimwa kama anavyo virusi vya ugonjwa wa Ebola pamoja na kwamba aliwaambia Manesi kwamba ametokea Liberia ambako kuna Ebola.
Screen Shot 2014-10-10 at 8.38.05 AM
Reverend Jesse Jackson akiwa na mama mzazi wa Duncan.
Ndugu mwingine wa kiume wa Duncan amesema mgonjwa wao hakuwa chini ya uangalizi mzuri kama ilivyotakiwa na alibaguliwa kwa sababu ya weusi wake, yani kuna wale Wagonjwa wazungu waliokutwa na Ebola waliwekewa uangalizi mzuri mpaka wakapona ila huyu sababu ni mweusi akatelekezwa.
Screen Shot 2014-10-10 at 8.37.39 AM
Hii picha ni Duncan akiwa na ndugu yake muda mfupi baada ya kuwasili Marekani kwenda kumuoa mchumba wake wa siku nyingi.
Screen Shot 2014-10-10 at 8.37.19 AM
Louise Troh mchumba wa Marehemu Duncan anaeonekana upande wa kulia.
Duncan aliekua na umri wa miaka 42 muda mfupi kabla ya kufariki alikua akitaka kumuona mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka 19 anaeonekana kwenye picha hapa chini lakini haikuwezekana.
Screen Shot 2014-10-10 at 8.54.47 AM
Hawa kwenye picha hapa chini ni watu waliobobea kwenye usafishaji na waliitwa kufanya usafi kwenye nyumba aliyokua anakaa Duncan huko Dallas Texas kabla ya kwenda Hospitali ambapo vitu vyake kama mashuka na mataulo vilibaki kwenye nyumba hiyo kwa siku tano baada ya yeye kupelekwa Hospitali.
Screen Shot 2014-10-10 at 8.56.18 AM