Kuna ajali nyingine hazijazoeleka kwenye macho ya watu wengi katika maisha ya uhalisia labda kwenye movie, hii inaweza kuwa moja wapo ambayo imetokea Dar es salaam maeneo ya Mwenge.
Dereva Yusuf Ally Massiru anasema alikua anatoka Mwenge kumshusha mke wake mpenzi kazini na kisha akawa anarudi Mbezi Beach kutokea Mwenge lakini sekunde chache Mwanajeshi akasimamisha magari ili kuvusha Wanafunzi barabara.
Wakati amesimama akaona kwenye kioo kuna lori linakuja nyuma kwa spidi na linapita upande mwingine wa barabara bila kujua kulikua kuna Wanafunzi wanavushwa hivyo Yusuf akaamua ajitoe muhanga kwa kuisogeza gari ili lori limkwepe alafu watoto wasigongwe.
Hapo ndipo mpango wake ulipofanikiwa na Lori likamkwepa ila katika kupanda ukuta wa pembeni likashindwa kuhimili na ikabidi limuangukie na kumbana.
Anakwambia alilaliwa kama unavyoona kwenye picha kuanzia saa 12 asubuhi mpaka saa mbili kasoro asubuhi ndio Wanajeshi wakasaidia mpaka akatoka pamoja afande Solomon mkuu wa kituo cha Osterbay aliesaidia sana manake alikuja mpaka eneo la tukio akakimbia mpaka fire tena na kurudi kwenye eneo la tukio mpaka akaagiza mtungi wa gesi ili Yusuf aweze kupumua manake alianza kukosa hewa kifusi kilikua kimmefukia sehemu kubwa.
Wakati wanataka kulitoa lori minyororo ilikatika na lori ndio likazidi kumbana kifuani ambapo wakati wote huo shingo na mgongo vilikua vimebanwa ila miguu ndio ilikua na uhuru kidogo.
Baadae Wanajeshi na nguvu zao ndio walifanikiwa kumtoa hiyo ikiwa ni saa mbili kasoro asubuhi akapelekwa hospitali ya Lugalo kisha Aga Khan Hospitali na kuruhusiwa na sasa yuko nyumbani pamoja na maumivu ya kupasuka kidole ambacho alishonwa.
Yusuf ameiambia millardayo.com kwamba akiwa mwenyewe tu kwenye gari muda wote aliokua kabanwa alikua na uwezo wa kuongea pamoja na kupiga simu ambapo alimpigia simu mke wake pamoja na mama mzazi.
No comments:
Post a Comment