Friday 4 April 2014

MAJALADA YA KESI YA RUSHWA YA MBUNGE WA CHADEMA ROSE KAMILI YAKAMILIKA

Jalada la kwanza ni la tuhuma za kutoa rushwa zinazomkabili mbunge ambazo zilitokana na walinzi wa CCM kumkamata wakidai alikuwa akifanya uhalifu huo na pili linahusu madai ya Kamili kuwa alitekwa, kudhalilishwa na kupigwa na wana-CCm hao. 
Iringa. Majalada mawili yaliyofunguliwa na polisi katika sakata la kutekwa kwa Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Rose Kamili yamefikishwa kwa Mwanasheria wa Serikali kwa ajili ya hatua zaidi.
Kamili alituhumiwa kutoa rushwa kwa wananchi wa Kijiji cha Kitayawa, Kata ya Luhota wakati wa uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga.
Jalada la kwanza ni la tuhuma za kutoa rushwa zinazomkabili mbunge ambazo zilitokana na walinzi wa CCM kumkamata wakidai alikuwa akifanya uhalifu huo na pili linahusu madai ya Kamili kuwa alitekwa, kudhalilishwa na kupigwa na wana-CCm hao.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Wankyo Nyigesa alisema jana kuwa uchunguzi wa polisi umekamilika na wameyafikisha majalada hayo kwa Mwanasheria wa Serikali kwa ajili ya hatua zaidi.

No comments: