
WATU  sita  akiwemo kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Rachel Kasanda wamenusurika  vifo baada ya magari waliokuwa wamepanda kugongana uso kwa uso katika eneo la power station lililopo Namtumbo  Mjini mkoa wa Ruvuma.
Akizungumza ofisini kwake kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma George  Chiposi alisema kuwa tukio hilo  limetokea july 8 mwaka huu majira ya saa 12:30 asubuhi  huko katika eneo la power station Namtumbo.
Alifafanua zaidi  kuwa inadaiwa  gari lenye namba za usajiri STK 6534 Nissan Patrol ambalo  lilikuwa linaendeshwa na John Dominic Nchimbi (46) mkazi wa songea mjini iligongana uso kwa uso  na gari nyingine  yenye namba za usajiri T 493 ANU Rover4  amabayo ilikuwa ikiendeshwa na Ally  Juma (29) mkazi wa Namtumbo  na kusababisha magari yote mawili kuharibika .
Alisema kuwa uharibifu uliotokea  kwenye magari hayo ni kwamba  kila gari liliharibika  lakini watu wote walikuwemo kwenye magari hayo walitoka salama.
Alieleza zaidi kuwa  gari lenye namba za usajiri STK 6534 Nissan Patrol  ilikuwa  inatoka
 kumchukua mkimbiza mwenge kitaifa Rachel kwenye hotel alikokuwa 
amefikia kwenda eneo la kijiji cha suruti ambako mwenge ulikuwa umelala 
tayari kwa kuanza safari  ya kwenda wilayani Tunduru.
Amewataja abiria waliokuwemo kwenye gari  hiyo aina ya rover4 iliyokuwa ikiendeshwa  na Ally Juma kuwa ni Omary Ngonyani (23) mkazi wa songea, Irene Kitula  (38) mkazi wa Namtumbo, Sekera Mwamwezi  mkazi wa Namtumbo na kwenye gari aina ya Nissan iliyokuwa ikiendeshwa na Nchimbi ilimbeba mkimbiza mwenge kitaifa Rachel .
 
No comments:
Post a Comment