Sunday, 6 July 2014

MASHABIKI WA MBEYA CITY TAWI LA SIDO WAIFANYIA SHEREHE TIMU YAO.

Laizer Ngela Katibu wa Mbeya city tawi la Sido aliesimama akitoa neno la shukrani kwa wachezaji wa Mbeya city
Abubakari Masoli Meneja matukio wa TBL  Mbeya akitambulisha kinywaji cha Grand Malt kwa wachezaji wa Mbeya City
Mwenyekiti wa Timu ya Mbeya City, Musa Mapunda, akizungumza kwa niaba ya Meya wa Jiji la Mbeya, Atanus Kapunga katika sherehe hizo
katibu wa Mbeya City, Emmanuel Kimbe akiongea na mashabiki wa Mbeya city wa tawi la Sido
Mc Lambat
Meneja wa Hotel ya GR  Sam Erick 
MASHABIKI wa Timu ya Mbeya City tawi la Sido jijini Mbeya wameipongeza timu hiyo kwa mafanikio waliyoyapata katika Msimu uliopita wa Ligi kuu Bara uliomalizika kwa timu hiyo kuibuka mshindi wa tatu.
Pongezi hizo zilitolewa jana katika Sherehe iliyoandaliwa na Tawi hilo zilizofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Gr iliyopo Soweto jijini Mbeya na kudhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) iliyohudhuriwa na wachezaji wote wa Mbeya city pamoja na viongozi na mashabiki.
Wakizungumza katika sherehe hizo. Mashabiki hao walisema timu hiyo imeweza kuzitikisa timu kongwe na kubwa hapa nchini hivyo hawana budi kutoa ushirikiano kwa timu yao katika msimu ujao ili iweze kuibuka katika nafasi mbili za juu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Timu ya Mbeya City, Musa Mapunda, akizungumza kwa niaba ya Meya wa Jiji la Mbeya, Atanus Kapunga, alilipongeza Tawi la Sido kwa kuonesha uzalendo kwa timu yao na kuwa chachu ya mafanikio ya timu.
Alisema mashabiki wa Mbeya city tawi la Sido limekuwa likishiriki shughuli nyingi za timu ikiwa ni pamoja na kusafiri na timu kila timu inapoenda kwa gharama zao wenyewe tofauti na matawi mengine ambayo hutaka kuchangiwa.
Alisema mafanikio ya Mbeya city hayapendwi na watu wengi hususani wapinzani wao hivyo ni vema mashabiki wakaunga mkono kwa nguvu zote ili kuhakikisha timu inafanya vizuri tofauti na wao wanavyotaka.
Aidha katika Sherehe hizo Wachezaji wa Mbeya city walitambulishwa mbele ya mashabiki pamoja na kukabidhiwa zawadi zilizotolewa na Abubakar Masoli,ambaye ni Meneja matukio wa Kampuni ya Bia (TBL) Mbeya.
Naye katibu wa Mbeya City, Emmanuel Kimbe, alisema shughuli zote za kiuchumi za timu hiyo zitashirikisha moja kwa moja mashabiki na matawi pamoja na Halmashauri ili kuhakikisha ushirikiano unadumu kwa mafanikio ya timu.

No comments: