Sunday, 6 July 2014

Hii ndio idadi ya waliokufa baada ya mji wa Lamu Kenya kukumbwa na mashambulizi ya risasi.

lamu

Wizara ya mambo ya ndani Kenya imesema kuwa zaidi ya watu 29 wameuawa katika mashambulizi mawili tofauti katika makazi ya Pwani ya nchi hiyo karibu na mpaka wa Somalia.
Watu 20 waliuawa katika eneo la Gamba kaunti ya Tanariver huku tisa wengine wakipoteza maisha kufuatia mashambulizi ya kufyatuliana risasi katika kituo kimoja cha kibiashara kaunti ya lamu karibu na mpaka wa Somali.
lamu2

Kundi la wapiganaji wa Al shabaab limekiri kutekeleza mashambulizi hayo ambapo inadaiwa watu walikuwa wakiangalia mechi za kombe la dunia wakati wa tukio hilo.
Mashuhuda wanasema watu kadhaa wenye silaha walifika katika kituo cha biashara katika eneo la Hindi jimbo la Lamu, mapema siku ya jumamosi jioni na kuanza kufyatua risasi za moto.
Mashambulizi katika eneo Lamu mapema mwezi uliopita yalisababisha vifo vya watu 60, wakati wanamgambo wa al shaabab wakivamia hoteli na vituo vya polisi.

No comments: