Bunge la bajeti linaendelea bungeni mjini Dodoma ambapo sasa ni zamu
ya wizara ya fedha na uchumi. Bajeti yake imewasilishwa na waziri wa
fedha Saada Mkuya Salum ambapo bajeti yake imepita huku suala la deni la
taifa likiendelea kuumiza vichwa vya wabunge wengi kwa kuendelea kukua
siku hadi siku.
Suala hilo limeonekana kuwashtua wabunge wengi akiwemo Mheshimiwa Christina Lissu ambaye anasema fedha zinazokopwa na kuongeza deni la taifa zimekuwa hazitumiki katika miradi ya maendeleo.
Mhe. Lissu anasema “Mheshimiwa spika deni la taifa, tumeangalia hotuba ya kamati ya wizara hii ikieleza kwamba deni la taifa limekua kutoka trilioni 21 hadi 29 ikiwa ni ongezeko la trilioni 8 tu kwa miaka 7, kukopa ni sahihi na nchi yoyote inakopa lakini je fedha tunazokopa zinaenda katika miradi ya maendeleo? Mbona ukuaji huu wa deni hauendani na fedha zinazoelekezwa katika miradi ya maendeleo?.”
“Kwa mwaka huu karibu miradi yote ya maendeleo imepelekewa fedha chini ya asilimia 50, mbona ukuaji wa deni hauendani na fedha zilizoenda kwenye matumizi ya maendeleo? inawezekana tunakopa na tuaambiwa deni ni stahimilivu lakini kama fedha haiendi kupunguza matatizo ya wananchi inakuwa haina maana kukopa.”
Suala la kuchelewesha fedha zinazotengwa kwa ajili ya bajeti ya miradi mbalimbali limeonekana kuwagusa wabunge wengi ambapo Mhe. Asupta Mshana anasema;
“Kumekuwepo na tatizo kubwa la fedha tunazoidhinisha kama bunge kutotolewa kwa wakati na kufanya kazi kama zilivyopangiwa, tatizo ni kwamba tunaandaa bajeti kwa kutabiri bila kuwa na fedha mkononi. Ni vyema tukabadilisha utaratibu wa kuandaa bajeti zetu badala ya kuwa na Cash bajeti tuwe na Capital bajeti”
Pamoja na jitihada za serikali kupitia kukusanya kodi je mikakati ya ukusanyaji kodi inatosha? Mhe. David Kafulila anasema;
“Tufike mahala tuwe na mkakati wa kutosha kuhakikisha maeneo yote ambayo hatukusanyi kodi tunakusanya. Tumezungumza mara kadhaa juu ya watanzania kuashiriki kwenye uchumi wa nchi yao kwa kupitia masoko ya mitaji katika soko la hisa DSE ili watanzania washiriki kwenye uchumi wao, tusiwanyime fursa wazawa kushiriki katika uchumi wao.”
Wakati Serikali ikiendelea kubanwa juu ya suala hilo, Waziri Kivuli wa Fedha, James Mbatia amesema ukiligawanya deni hilo kwa idadi ya Watanzania milioni 45, kila mwananchi atakuwa anadaiwa Sh600,000.

No comments:
Post a Comment