Thursday, 5 June 2014

Ripoti mpya ya waliokufa kutokana na Ebola nchini Guinea.

ebola

Umeshawahi kusikia kuhusu ugonjwa wa Ebola ambao umekuwa ukisumbua nchi kadhaa za Afrika na kusababisha vifo. Mpaka sasa takribani watu 208 wamepoteza maisha kutokana na virusi vya ugonjwa huo nchini Guinea kwa mujibu wa shirika la afya duniani.
Ripoti mpya iliyotolewa inaonyesha kuwa watu 21 wamekufa na watu 37 wamegundulika kupata virusi vya ugonjwa huo kati ya Mei 29 na June 1 mwaka huu na kufanya idadi kamili ya wagonjwa wa Ebola katika Ukanda wa Afrika Magharibi kufikia 328.
ebola2

Hakuna tiba wala kinga ya ugonjwa huo unaosababishwa na virusi hatari.
Zaidi ya nusu ya vifo vipya vilivyotokana na ugonjwa huo vimetokea katika Jimbo la Guekedou ambako ugonjwa huo umesambaa.
Watu watatu wamethibitishwa kupoteza maisha na wengine 10 kupata Virusi vya ugonjwa huo karibu na Sierra Leone na wengine 10 nchini Liberia.
Wataalamu wa afya wanasema moja ya sababu za kuongezeka kwa vifo ni kutokana na watu kukataa kwenda hospitali kwa ajili ya matibabu na kufuata tiba kwa waganga wa jadi.

Ukuaji deni la taifa waumiza vichwa

Bunge la bajeti linaendelea bungeni mjini Dodoma ambapo sasa ni zamu ya wizara ya fedha na uchumi. Bajeti yake imewasilishwa na waziri wa fedha Saada Mkuya Salum ambapo bajeti yake imepita huku suala la deni la taifa likiendelea kuumiza vichwa vya wabunge wengi kwa kuendelea kukua siku hadi siku.
Suala hilo limeonekana kuwashtua wabunge wengi akiwemo Mheshimiwa Christina Lissu ambaye anasema fedha zinazokopwa na kuongeza deni la taifa zimekuwa hazitumiki katika miradi ya maendeleo.

Picha no 6(2)
Mhe. Lissu anasema “Mheshimiwa spika deni la taifa, tumeangalia hotuba ya kamati ya wizara hii ikieleza kwamba deni la taifa limekua kutoka trilioni 21 hadi 29 ikiwa ni ongezeko la trilioni 8 tu kwa miaka 7, kukopa ni sahihi na nchi yoyote inakopa lakini je fedha tunazokopa zinaenda katika miradi ya maendeleo? Mbona ukuaji huu wa deni hauendani na fedha zinazoelekezwa katika miradi ya maendeleo?.”
“Kwa mwaka huu karibu miradi yote ya maendeleo imepelekewa fedha chini ya asilimia 50, mbona ukuaji wa deni hauendani na fedha zilizoenda kwenye matumizi ya maendeleo? inawezekana tunakopa na tuaambiwa deni ni stahimilivu lakini kama fedha haiendi kupunguza matatizo ya wananchi inakuwa haina maana kukopa.”
Suala la kuchelewesha fedha zinazotengwa kwa ajili ya bajeti ya miradi mbalimbali limeonekana kuwagusa wabunge wengi ambapo Mhe. Asupta Mshana anasema;
“Kumekuwepo na tatizo kubwa la fedha tunazoidhinisha kama bunge kutotolewa kwa wakati na kufanya kazi kama zilivyopangiwa, tatizo ni kwamba tunaandaa bajeti kwa kutabiri bila kuwa na fedha mkononi. Ni vyema tukabadilisha utaratibu wa kuandaa bajeti zetu badala ya kuwa na Cash bajeti tuwe na Capital bajeti”
Pamoja na jitihada za serikali kupitia kukusanya kodi je mikakati ya ukusanyaji kodi inatosha? Mhe. David Kafulila anasema;
“Tufike mahala tuwe na mkakati wa kutosha kuhakikisha maeneo yote ambayo hatukusanyi kodi tunakusanya. Tumezungumza mara kadhaa juu ya watanzania kuashiriki kwenye uchumi wa nchi yao kwa kupitia masoko ya mitaji katika soko la hisa DSE ili watanzania washiriki kwenye uchumi wao, tusiwanyime fursa wazawa kushiriki katika uchumi wao.”
Wakati Serikali ikiendelea kubanwa juu ya suala hilo, Waziri Kivuli wa Fedha, James Mbatia amesema ukiligawanya deni hilo kwa idadi ya Watanzania milioni 45, kila mwananchi atakuwa anadaiwa Sh600,000.

Avaa kama Rambo na kufanya mauaji ya maafisa watatu wa polisi.

rambo

Wahalifu kila siku wanakuja na mbinu mpya ambapo Polisi nchini Canada wanamsaka mtu hatari mwenye silaha ambaye amevaa mavazi kama ya muigizaji wa filamu za mapigano Rambo. Mtu huyo amewaua kwa kuwapiga risasi maafisa watatu wa polisi na kujeruhi wengine wawili katika tukio hilo la pamoja.
Mashambulizi hayo ya risasi yamefanyika wakati polisi walilipokea simu juu ya mtu aliyekuwa na silaha Kaskazini mwa mji wa Moncton katika Jimbo la Pwani ya Mashariki ya New Brunswick.
rambo2

Maafisa hao watatu waliokwenda katika eneo hilo waliuwawa na wengine kupata majeraha lakini sasa wapo katika hali nzuri.
Mtuhumiwa huyo mwenye umri wa miaka 24 Justin Bourque, kutoka mjini Moncton, anadaiwa kuwa alibeba silaha nzito za mapigano pamoja na visu.
rambo3

Polisi waliweka picha ya mwanaume huyo akiwa amevaa mavazi ya kijeshi na kushika bunduk

yule trafic wa Kenya alievaa sketi fupi?kaja na hii tena.

TZA AFISA WA POLISI KENYA
Yule trafiki wakike wa Kenya ambae kwa sasa Wakenya wengi wanamuita Koplo Linda Okelo ameingia tena kwenye headlines huko huko Kenya na kwa sasa ameamua kwenda mahakamani kupinga hatua ya kamati ya kinidhamu iliyowekwa.
Hatua hiyo ni ya kuchunguza madai ya kuvaa sketi fupi ambayo imesemwa kuwa ilikua nje ya maadili ya kazi na sheria za Jeshi hilo la Polisi la nchini Kenya.
Kupitia kwa wakili wake Tom ojienda Koplo Lindah amesema kwamba hakufanya kosa lolote kuvaa sketi hiyo hadi kulazimika kuundwa kamati ya kumchunguza na kutoa maelekezo ya adhabu anayostahili.
Lindah amesema kwamba asubuhi ya April  26 alifanya mkutana na OCPD wa kituo cha kiambu ili kuelekezwa,ingawa mkuu huyo wa polisi hakusema lolote kuhusiana na mavazi aliyovaa.
Ingawa May 2 Lindah alichukuliwa hatua za kinidhamukwa kosa la kuvaa mavazi yaliyombana kulingana na sheria za huduma za polisi-alivyo kuwa amevalia sketi fupi iliyombana saa saba mchana nje ya tawi la benki ya KCB lililopo kiambu.
Linda amedai kwamba sketi iliyo zua utata alikabidhiwa na afisa anaye shughulika na sare za polisi mwaka 2003 na amekua akivaa kila siku na mabosi wake hawakuwahi kulalamika kabla ya tarehe 26 Aprili.
Wakili wake Ojienda amesema kwamba wakati wa kikao cha kamati hiyo may 7 na may 9 Bii Okelo alichukuliwa hatua kimakosa kwani hakukua na sababu za kumuhukumu kulingana na mavazi yake,kesi yake itatajwa june 12 mwaka huu.

Baada ya mzozo wa muda mrefu juu ya umiliki wa nyimbo za Bob Marley, hiki ndicho kilichoamuliwa.

bob-marley-principal

Mzozo wa kisheria juu ya nani anayemiliki baadhi ya nyimbo maarufu za reggae duniani za Bob Marley umemalizika mjini London.
Nyimbo hizo zilizotungwa na kuimbwa na msanii Bob Marley zimekuwa ziking’ang’aniwa na kampuni 2 pinzani juu ya umiliki wao.
bob-marley2

Jaji katika mahakama kuu, Richard Meade alikata kesi ambapo kampuni ya Cayman Music ilikuwa inadai kumiliki nyimbo 13, miongoni mwao wimbo uliopata umaarufu ‘No Woman, No Cry’ kuwa haina haki nazo tena.
Kampuni hiyo ilikuwa imedai kuwa nyimbo hizo hazikujumuishwa walipouza baadhi ya haki zake kwa kampuni nyingine mnamo mwaka wa 1992.
Kampuni ya Cayman imesema kuwa Bob Marley aliandika nyimbo hizo chini ya majina tofauti, lakini Jaji ameamua kuwa bado kandarasi waliouzia inafunika nyimbo zote hizo.
Bob Marley alifariki mwaka wa 1981 baada ya kuugua maradhi ya saratani kwa muda.

Shabiki anunua nyumba ya Whitney Houston.

fan

Mapenzi yaliyopitiliza ya shabiki wa muziki wa Marehemu Whitney Houston yamemfanya kununua nyumba ya mwanamuziki huyo na kuahidi kuitunza kwa ajili yake.
Nyumba hiyo ya Whitney iliyopo katika mji wa Mendham huko New Jersey imeuzwa kwa takribani dola milioni 1.5 kwa Matthew Krauthamer, ambaye ni shabiki wake na amedai kuwa hataki kuibadilisha nyumba hiyo yenye ukubwa wa hekari tano.
Whitney-Houston

Nyumba hiyo ambayo Whitney hakuishi kwa muda wa miaka mitano kabla ya kifo chake kilichohusishwa na dawa za kulevya kilichotokea February mwaka 2012 ina jumla ya vyumba vitano, garage sita za magari.
Wakati mwanamuziki huyo ananunua nyumba hiyo aliiongezea studio ya kurekodi muziki, chumba cha michezo, chumba cha burudani, uwanja wa mchezo wa Tennis na nyumba ya bwawa la kuogelea na mmiliki huyo mpya amesema anataka kuifanya nyumba hiyo ya kiburudani zaidi.

BAADA YA MBINGA DSM NA SONGEA DOM SASA NI ZAMU YA MBINGA MBEYA NA SUPER FEO EXPRESS

 basi dogo la kampuni ya mabasi yenye ubora wa kuaminika kwa kusafirisha abiria mkoa wa ukanda wa kusini(super feo) limeanza safari ya mbinga mbeya kupitia songea,njombe na makambako ili kurahisisha usafiri kwa wakazi wa mbinga hatua hii imechukuliwa na kampuni hii baada ya safari ya mbinga dsm na ile ya songea dodoma kukubaika na wasafiri wa ukanda wa kusini sasa tutegemee safari nyingine mpya baada ya hii


Tuesday, 3 June 2014

Uchaguzi mkuu wafanyika Syria

Uchaguzi mkuu wafanyika Syria wapiga kura wakisema wanaumuunga mkono Rais Asaad

Taifa la Syria linafanya uchaguzi mkuu ambao upinzani umepuuza. Rais Bashar al-Assad anatarajiwa kupata ushindi kwa urahisi dhidi ya wapinzani wake wawili walioidhinishwa na serikali .
Upinzani unaoungwa mkono na mataifa ya magharibi umepinga uchaguzi huo na kuususia huo .
Kwa mara ya kwanza katika miaka hamsini, familia ya Assad inakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa wagombea wawili, lakini Rais Bashar al-Assad, ambaye ashapiga kura na mkewe Asmaa, anatarajiwa kushinda uchaguzi huo.
Wakazi wa Damascus wameambia BBC kuwa wanampigia kura Rais Assad kwa sababu anapambana dhidi ya tisho la ugaidi.
Katika maeneo ambayo hana udhubiti, uchaguzi haufanyiki.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa ingawa kila mtu ambaye ameongea naye anaunga mkono Assad, serikali imechukulia uchaguzi huu kwa uzioto huku ikiwasafirisha wapiga kura kwa mabasi kupiga kura.

Instagram yafuta picha za Uchi

                                                 
                                   Kevin Systrom afisaa mkuu mtendaji wa Instagram
Mmoja wa waasisi wa mtandao wa kijamii wa Instagram, ameambia BBC kuwa sheria zake kuhusu picha za uchi hazimbagui mtu yeyote.
Kampuni hiyo imekosolewa vikali kwa kwa kuondoa picha za wanawake walio nusu uchi kwenye mtandao huo.
Lakini Afisaa mkuu mtendaji wa mtandao huo wa kijamii, Kevin Systrom, amesema kuwa sheria hizo zinalenga kuhakikisha kuwa vijana na watu wazima wanaotumia mtandao huo wako salama.
Masharti ya matumizi ya mtandao wenyewe, yanasema: 'Mtu haruhusiwi kuweka picha za watu walio nusu uchi na picha zenye mada ya ngono. ''
Matamshi yake yanakuja baada ya mwanawe muigizaji maarufu, Bruce Willis, Scout Willis kuweka picha yake kwenye mtandao huo akiwa nusu uchi bila kitu kifuani.
Picha hiyo iliondolewa kwenye mtandao huo na wamiliki wa mtandao na hapo ndipo malalamiko yalianza kuibuka.
Muimbaji Rihanna, ambaye alikuwa na wafuasi milioni 1.3 aliunga mkono kampeini hiyo kabla ya kufunga akaunti yake.
Wamiliki wa mtandao huo wanasema sheria zinapaswa kufuatwa na kila mtu awe mtu mashuhuri au vinginevyo.
"lengo letu ni kuhakikisha kuwa Instagram, ni mahala salama kwa kila mtu , awe maarufu au la. ''
"tunapaswa kuwa na sheria na kuhakikisha kuwa kila mtu anafuata sheria hizo. Bila shaka tunapata changamoto nyingi lakini tutnaedneklea kusisitiza umuhimu wa sheria kufuatwa, '' alisema Systrom
Huku umaarufu wa mtandao huo ukiendelea kuimarika, mtandao huo umekosolewa kuhusiana na baadhi ya picha zinazochapishwa humo . Pia mtandao wenye umebana baadhi ya maneno yanayohusiana na madawa ya kulevya.
Instagram ilinunuliwa na Facebook mwaka 2012

Utata kuhusu 'White Widow' Kenya


Uchunguzi unaohusisha vitengo vitatu vya serikali ya Kenya umeanzishwa kufuatia madai ya mtoro wa ugaidi anayesakwa duniani Samantha Lewthwaite, maarufu kama 'White Widow' , anayedaiwa kuonekana katika eneo la Lamu pwani ya Kenya.

Maafisa wa uchunguzi wa jeshi la Kenya kwa ushirikiano na maafisa wengine kutoka idara ya polisi na wizara ya usalama wa ndani wanachunguza madai kuwa maafisa wa polisi mjini Lamu walimpa ulinzi mama mmoja mzungu, ambaye alitoweka baada ya maafisa wa forodha na uhamiaji kumzuia kuondoka Kenya na kuingia nchini Somalia.
Ripoti zinasema kuwa polisi walimpa ulinzi mama huyo aliyedai kufanya kazi na shirika moja la kimataifa na alitaka kutembelea kambi ya wanajeshi wa Kenya nchini Somalia.
Alipofika eneo la mpakani la Kiunga maafisa wa uhamiaji walihoji uhalali wa stakabadhi zake na hivyo kumzuia kuondoka.
Mara tu baada ya tukio hilo, mama huyo alitoweka hadi sasa hajulikani aliko.
Msemaji wa majeshi ya Kenya, Willy Wesonga amethibitisha kuwa kundi la majasusi wamekabidhiwa jukumu la kuchunguza ikiwa kweli mwanamke huyo ni Samantha Lewthwaite na ikiwa ndiye, ni kwa nini alitaka kuzuru kambi ya wanajeshi wa Kenya.
Kamanda wa polisi katika kaunti ya Lamu, Leonard Omollo, amethibitisha kuwa maafisa wake walimpa ulinzi mama mmoja mzungu. Amesema wao hawakuwa na wasi wasi kwa kuwa aliwapa stakabadhi za kujitambulisha ila wao hawakuwa na hofu kuwa ni gushi.
Polisi pia wanalitafuta gari ambalo alikuwa amelikodisha baada ya kuthibitisha kuwa gari lilo hilo ndilo lililotumika majuma mawili yaliyopita katika shambulio dhidi ya wanajeshi wa Kenya ambapo wawili waliuawa na wengine kujeruhiwa.
Samantha aliwahhi kudaiwa kuhusina na mashambuliai ya kigaidi yaliyokumba jengo al kifahari la Kenya Westgate mwaka jana.

KWENYE NJAA KALI CHOCHOTE KINAWEZEKANA ASKARI FEKI NA BOSS WAKE FEKI WAKAMATWA IRINGA


Vijana  wanaotuhumiwa  kufanya utapeli  mkoa  wa Iringa na Morogoro kwa kujifanya maofisa wa  polisi mmoja  kulia akijifanya askari polisi na kushoto akijifanya ni mkuu wa  jeshi la polisi mjini wakiwa  chini ya ulinzi wa polisi mjini Iringa leo

June 3, 2014 Magazeti yanasemaje? soma hapa

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.