Tuesday, 27 May 2014

Hiki ndio kiwanda kikubwa cha magari kilichofungwa India, madeni yatajwa kuwa sababu.

Ambassador2

Kampuni kubwa ya utengenezaji wa magari aina ya Ambassador ya nchini India imefunga huduma zake za uzalishaji kwa madai ya kugubikwa na madeni na kukosekana na mahitaji ya ya gari hilo ambalo liliuzwa sana na kuweka matabaka katika nchi hiyo kutokana na gharama zake.
Kiwanda hicho cha Hindustan ambacho ni cha zamani zaidi kuliko vyote nchini humo imefunga huduma zake katika Jimbo la Uttarpara Magharibi mwa Bengal ambako imekuwa ikitengeneza magari ya aina hiyo tangu mwaka 1957.
Ambassador car, India

Afisa mkuu wa kiwanda hicho amesema kuwa kazi katika katika kiwanda hicho zimesitishwa na wamefanya hivyo kuhakikisha kiwanda hicho hakitumii fedha zaidi na kuwafanya kuweka mipango mipya ya kukirudisha.

No comments: