Watu
mbalimbali wenye magonjwa wakimiminika kwenye maji ya bwawa nchini
Nigeria na kuoga wakiwa na imani ya kuponywa magonjwa yao.
WANADAMU wanazidi
kuegemea kwenye imani utata! Hivi karibuni, watu mbalimbali wenye
magonjwa wamekuwa wakimiminika nchini Nigeria na kuoga maji ya bwawa
yanayodaiwa yanaponya magonjwa papo hapo.
Watu hao wakiwemo wazee, vijana waume kwa wake na wenye magonjwa
mbalimbali wamekuwa wakizama kwenye maji hayo kwa urefu wa futi tatu
hadi nne, wengi wakiwa uchi au nguo za ndani tu.Wengine huchota maji hayo na kuosha sehemu yenye tatizo hasa wale wenye kushindwa kuona au wenye vidonda sugu kama vile kansa, Ukimwi nakadhalika.
Bwawa hilo limepewa jina la Orimiri lipo umbali wa kilomita 3 kutoka mji
wa Nachi, Enugu nchini humo na liligunduliwa na watu wa Kabila la
Fulani.
Tangu kugunduliwa kwa bwawa hilo, zaidi ya watu 3000 wameshafika kuyaoga maji hayo kuanzia asubuhi hadi saa 12 jioni.
Hata hivyo, hakuna taarifa za moja kwa moja na uwazi kwamba watu wamepokea uponyaji.
Nigeria ni nchi yenye matukio mengi ya kiimani licha ya mambo ya kisiasa ambapo mpaka sasa wananchi wake wamekuwa wakikumbana nayo.
Nigeria ni nchi yenye matukio mengi ya kiimani licha ya mambo ya kisiasa ambapo mpaka sasa wananchi wake wamekuwa wakikumbana nayo.
Wananchi wakiwa wamejaa bwawani kama kwa Babu wa Samunge.
Baadhi ya viongozi wa dini wamekuwa wakiwaambia waumini wao kuamini zaidi katika uponyaji wa Mungu.
Nchini Tanzania, miaka ya karibuni aliibuka Mchungaji Ambilikile
Masapile ‘Babu wa Samunge’ akidai ana maji ambayo mtu mgonjwa akinywa
anapata uponyaji.
Watanzania wengi, wakiwemo viongozi wa serikali walimiminika kwenye
Kijiji cha Samunge, Loliondo kunywa kikombe chenye maji hayo lakini
baadaye ilikuja kubainika kwamba, hakukuwa na uponyaji wowote zaidi ya
kumwachia babu huyo utajiri.