Friday 28 November 2014

mkusanyiko wa Stori kubwa muhimu za Magazeti ya leo Novemba 28,2014

JAMBOLEO
Wakati mjadala wa Escrow ukiendelea Bungeni Dodoma,zNi halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa imedaiwa kutawala miongoni mwa wabunge ili kuhakikisha wanaotuhumiwa na wizi wa fedha hizo hawawajibishwi kama kamati ya bunge ya hesabu za Serikali PAC ilvyopendekeza.
Wakizungumza kwa nyakati togfauti katika viwanja vya bunge ,baadhi ya wabunge wakiwa wa CCM na wanaounda PAC walionekana dhahiri kutoridhishwa na mwenendo wa mambo yanavyoendesha mara baada ya ripoti hiyo kusomwa.
Mbunge wa Mwibara Kangi Lugola alisema  imebainika safari hii rupia imepenyezwa kila konahali inayosababisha kuteka wabunge wengi na kudhoofisha mjadala.
“Lumbesa ikishaingia mahali hakuna kupitisha uzio,ukishapokea rushwa unakua kipofu,husikii lakini hatukubali jambo hilo.
Hamis Kigwangallah naye alisema ameshangazwa na kamati ya uomgozi ilivyofnya muda wa kuijadili ripoti hiyo kwa kuwa jana jioni manasheria mkuu alitarajiwa kutoa utetezi wake pia Waziri mkuu.
MWANANCHI
Askofu msaidizi wa jimbo la Bukoba Methodius Kilaini amekiri kupokea milioni80.5 kutoka kwa mkurugenzi wa VIP Engeneering,James Rugemarila akisema si mara yake ya kwanza kupokea fedha kuroka kwa mfanyabiashara huyo kwa kuwamara nyingi huwa anachangia  kwa uwazi miradi ya jamii.
Kilaini alisema Rugemarila hupendelea kuchangia miradi ya maendelezo kwa uwazi na si yeye pekee aliyempatia mchango kuna watu wengine wengiambao wamempatia michango na kazi yake yeye ni kuipokea na kuifikisha sehemu husika.
Alisema fedha hizo alizozipokea ni kwa ajili ya miradi inayoendeshwa na kanisa Karoliki na fedha zote anazopokea si siri na kuwatgaka wanaomuhofia kuwa ni miongoni mwa mafisadi wawafate wahusika.
“Ndiyonimepokea fedha na si mara ya kwanza amekua aitoa misaada kila wakati na hii si sirim,wafuateni wezi halisi si mimi”alisema.
MWANANCHI
Bunge la Afrika Mashariki limemsimamisha kwa siku 21 Spika wake Margaret Zziwa huku likifufua hoja ya kumwondoa kiongozi huyo madarakani ambayo iliwekwa kando April1 mw aka huu.
Bunge hilo pia liliafiki kauliya Mbunge kutoka Tanzania AbdulMwinyi ya kumzuia Dk ya kumzuia Spika Zziwa kujihusisha na shughuli zozote za  za nafasi ya Spika mpaka hapo uchunguzi dhidi ya tuhuma utakapokua umekamilikana na kuwasilishwa bungeni.
Uamuzi wa Bunge hilo ulifikiwa juzi mchana ikiwa ni hitimisho la mkutano wa saa nne ambao ulimchagua Mbunge kutoka Uganda Chris Opako kusimamia mchakato huo wa kumwondoa Zziwa madarakani  kwa mujibu wa uendeshaji wa Bunge hilo.
Msemaji wa bunge hilo Bobi Odiko alisema kusimamishwa kwa Spika Zziwa kunamaanishakwamba bunge hilo halitaweza kukutana tena kwa siku chache zilizobakia hadi pale kamati itgakapokua imemaliza kazi yake.
MWANANCHI
Watu 11 wamekufa papo hapo na wengine 25 kujeruhiwa baada ya basi dogo aina ya Coaster kugongana uso kwa uso na lori la mizigo aina ya scania katika kijiji cha Mkanyageni Wilaya ya Muheza,Mkoani Tanga.
Ajali hiyo ilitokea jana saa11 asubuhi wakati basi hilo lili[okua linatoka Tanga kwenda Lushoto na Lori hilo likitokea Lushoto kwendaTanga.
Kaimu Mganga mkuu wa Wilaya Peter Mwankai alisema miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika hospitali teule ya Muheza na tayari maiti saba zimetambuliwa na ndugu zao.
Alisema majeruhi 22 wanaendelea vizuri na wana endelea kupatiwa matatibabu katika hospitalihiyo chini ya uangalizi maalum.
NIPASHE
Jitihada za Serikali kuibadilisha nchi kuwa  miongoni mwa zile zenye malengo makuu ya maendeleo zinawea kutoleta mafanikio kutokana na bajeti ndogo inayotengwa kwa ajili ya kusimamia miradi mbalimbali.
Uwezo huo mdogo wa bajeti umesababisha miradi mingi ya Serikali kusuasua na mingine kufa,ingawa mfumo wa kiutendaji inaonyesha Tanzania imefanya vizuri kwa asilimia90.
Mratibu wa mradi wa Taifa wa kusimamia maendeleo ya Umoja wa soko la pamoja COMESA Cliford Tandaralisema kupitia ripoti ya utendaji imeonyesha kufanya vizuri kwani kwani sekta za umma kama Baraza la Mawaziri,Bunge na Mahakama ni mihili mikuu katika nchi kusimamiwa vizuri hasa kiutendaji.
Inadaiwa kuwa uchumi wa Tan zania ni moja ya uchumiunaokua kwa kasi duniani na kwamba katika miaka10 hadi15 iliyopita uchumi umekua kwa wastani wa asilimia 7.
NIPASHE
Uandikishaji wa wapiga kura katika Jiji la Dar essalaam umekumbwa na vurugu katika baadhi ya maeneo.
Wakazi wa maeneo mbalimbali walisema  ofisi zilizuka katika ofisi za Serikali za mitaa baada ya mawakala wa vyama kuingilia kati na kudai kuwa uandikishaji huo haukufuata utaratibu wa mipaka yao na ziliztulizwa na polisi waliokua wakilinda usalama katika vituo ya uandikishaji ambao walisimamia hadi muafaka upatikane.
Alisema kuwa vurugu hizo zimechukua saa tatu hali iliyochangia kusimamishwa kwa zoezi hilo ili kukaa na mawakala wa vyama na kujadili muafaka wa sehemu yenye matatizo  ya mipaka watajiandikisha wakati mwingine.

No comments: