Hii
inakuwa ajali ya kwanza kutokea wiki moja tangu kuzinduliwa kwa majengo
ya ghorofa pacha ya One World Trade Centre, New York Marekani.
Watu wawili wanaofanya shughuli za kusafisha vioo vya majengo makubwa na ghorofa, wamepata ajali wakati wakifanya shughuli hiyo katika moja ya ghorofa za One World Trade Centre na muda mfupi baadaye wakaokolewa na Askari wa Kikosi cha Zimamoto.
Kamba za lifti ambayo wanaitumia
kufanyia kazi hiyo zilinasa na kugoma kufanya kazi wakiwa ghorofa ya 69,
wakajikuta wanakaa bila msaada wowote kwa saa moja na nusu, huku wapita
njia walioshtushwa na tukio hilo wakiendelea kuwapiga picha ambazo
zimeenea mitandaoni.
No comments:
Post a Comment