Spika wa Bunge la Afrika Mashariki EALA, Margaret Zziwa
amesimamishwa kazi na Wabunge wa Bunge hilo kwa kile kinachoelezwa kuwa
amekuwa akiendeleza ubaguzi kwenye ajira, ufisadi na pia hana uongozi
bora.
Katika mahojiano aliyoyafanya na kituo cha BBC
amekana madai hayo na kusema malumbano yanayoendelea ndani ya Bunge
hilo yanatokana na siasa za chuki baina ya Wabunge na kusababisha Bunge
hilo kutimiza majukumu yake.
Uchunguzi unafanyika ili kujua kama madai yaliyopelekea kumsimamisha yalikuwa na ukweli wowote.
No comments:
Post a Comment