Septemba
21, 2013 ni moja ya siku ambazo zina kumbukumbu nzito ya majonzi kwa
watu wa Kenya, kutokana na kupata shambulizi la kigaidi liliposababisha
vifo vya watu zaidi ya 60 huku hofu kubwa ikitanda na kupelekea baadhi
ya maeneo ambayo huwa na mkusanyiko wa watu wengi Afrika Mashariki
ikiwemo Mlimani City Dar kuwekwa ulinzi wa hali ya juu.
Taarifa inayomhusu mtuhumiwa namba 1 wa kesi ya mashambulizi ya jengo la Westgate Samantha Lewthwaite ni kwamba ameuawa kwa kupigwa risasi.
Taarifa zinasema mtuhumiwa huyu ambaye alikuwa akifahamika kama “White Widow” ameuawa Ukraine katika mapambano ambapo alikuwa akipambana upande wa kikosi cha wapiganaji wa Aidar.
Samantha amekuwa akituhumiwa kuhusika na
matukio kadhaa ya mashambulizi ikiwemo la Westgate Kenya mwaka 2013
japo matukio hayo mengi haikuwahi kuthibitika juu ya ushiriki wake.
No comments:
Post a Comment