Thursday, 13 November 2014

AJALI TENA

MWANGA
Habari zilizotufikia kutoka Mwanga Mkoani Kilimanjaro zinasema kuna ajali mbaya imetokea maeneo ya Mwanga wakati basi la kampuni ya Mbazi Travellers lililokua likitokea Arusha kuelekea Dar es salaam kupinduka.

Taarifa  zinasema ajali hiyo ilitokea baada ya basi hilo kujaribu kulipita basi jingine huku kukiwa hakuna mtu aliyepoteza maisha lakini inasemekana kuna idadi kubwa ya majeruhi ambao walikimbizwa katika hospitali ya KCMC Moshi

No comments: