Sehemu mojawapo iliyokubwa na dhahama (PICHANI) hiyo ni eneo la Godegode na Gulwe, Mpwapwa ambapo reli hiyo kongwe iko hatarini kuharibika na kuhitaji ukarabati mkubwa na wa haraka sana.
Mwandishi wa habari hizi alijionea ugumu wa safari ya kufika katika eneo la tukio ili kushuhudia madhara makuwa yaliyosababishwa na mvua hizo.
Imedaiwa chanzo cha madhara hayo ni shughuli za kibinaadamu zinazoendelea katika milima ya Kibakwe ambapo visiki vya magogo vimekuwa viking’olewa na kusababisha mtiririko mkubwa wa maji kutokea katika milima hiyo.
Akielezea chanzo hicho mmoja wa waandisi wa SUMATRA ambaye hakutaka kutajwa jina lake kwa madai kuwa yeye si msemaji wa TRL wala SUMATRA alisema
ANGALIA PICHA ZAIDI…
“mtiririko wa maji ya mvua hujikita kwenye Culvert za barabara mpya ya Halmashauri ya Mpwapwa ambapo matundu yake yamejengwa chini ya kiwango na kusababisha mkondo wa maji kurudi kinyumenyume na kutafuna tuta la reli”

No comments:
Post a Comment