Kwa mujibu wa Meneja Uhusiano wa Tanesco, Badra Masoud, mgao unatokana na kuzimwa kwa mitambo ya kampuni ya Pan African iliyopo Songosongo.
“Mitambo hiyo itazimwa kwa sababu ya matengenezo ya lazima, hakuna jinsi ya kuzuia hali hiyo Tanesco tunasikitika sana kwa kuwa kutakuwa na upungufu mkubwa wa umeme kwenye gridi ya taifa,” alisema Masoud.
“Upungufu huo umesababishwa na matengenezo ya kiufundi yanayofanywa kwenye visima vya gesi, lengo ni kuboresha upatikanaji wa gesi ya kutosha kwenye visima hivyo.”
No comments:
Post a Comment