Taarifa iliyotufikia asubuhi hii inasema malori zaidi ya 40 yamezuia njia kufuatia tukio la kutekwa kwa madereva wenzao watatu wa malori na majambazi kisha kukatwa mapanga,na inasemekana baada ya tukio hilo kutokea polisi walichelewa kufika eneo la tukio.
Mbali na malori kuna mabus ya abiria na magari binafsi ambayo nayo hayawezi kupita kufuatia agizo la madereva hao ambalo wamesema hawaachii njia mpaka Mkuu wa Mkoa wa Tabora au Rpc afike,huku wakidai hilo limekua ni tatizo sugu eneo hilo kutokana na kutokea vitendo vya utekaji mara kwa mara.
Eneo hili linaitwa laziba lipo katikati ya mji wa Laziba na Nzega,ni kilomita 20 kutoka Nzega Mjini,madereva hao wa malori wameziba njia tangu saa 3 asubuhi hii,japo taarifa inasema tukio la kutekwa kwa madereva hao limetokea jana saa 3 usiku.
No comments:
Post a Comment