Kama
kila siku huwa unaingia facebook, whatsapp au instagram inawezekana
ukawa ulikutana na hii picha ya Askari Polisi ambao walipigwa picha
wakiwa wanakiss wakiwa ndani ya sare za jeshi hilo.
Sasa taarifa mpya iliyotoka baada ya hii picha kuzidi kusambaa ni kwamba Jeshi la Polisi Kagera limechukua maamuzi ya kuwafukuza kazi askari hawa wawili pamoja na mwingine mmoja ambae ndio aliipiga hii picha kupitia simu yake ya mkononi.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Henry Mwaibambe amewataja askari hao kuwa ni PC Asuma Mpaji Mwasumbi mwenye namba F.7788,PC Fadhili Linga mwenye namba G 2122 na PC Veronica Nazaremo Mdeme na wote walikuwa askari wa kikosi cha usalama barabarani wilayani Missenyi.
Kamanda Mwaibambe amezungumza na ITV
na kusema askari hao walitenda kosa hilo la fedhea kwa kupiga picha
kinyume na maadili ya jeshi hilo mwaka 2012 wakiwa kazini na kwamba PC
Fadhili ndiye aliyehusika na kupiga picha hizo kwa kutumia simu yake ya
mkononi na kuituma katika mitandao mbalimbali ya kijamii kitendo ambacho
ni kinyume cha maadili kwa sababu mbalimbali.
Mwaibambe amekiri kuwa picha husika inayoonekana kwenye mitandao ni picha halisi ambayo haijachakachuliwa hivyo ni wazi kila askari kujua maadili ya kijeshi yapo kisheria na askari yeyote anafundishwa namna ya kuishi katika maisha ya utumishi wa jeshi la Polis
Sasa taarifa mpya iliyotoka baada ya hii picha kuzidi kusambaa ni kwamba Jeshi la Polisi Kagera limechukua maamuzi ya kuwafukuza kazi askari hawa wawili pamoja na mwingine mmoja ambae ndio aliipiga hii picha kupitia simu yake ya mkononi.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Henry Mwaibambe amewataja askari hao kuwa ni PC Asuma Mpaji Mwasumbi mwenye namba F.7788,PC Fadhili Linga mwenye namba G 2122 na PC Veronica Nazaremo Mdeme na wote walikuwa askari wa kikosi cha usalama barabarani wilayani Missenyi.
Mwaibambe amekiri kuwa picha husika inayoonekana kwenye mitandao ni picha halisi ambayo haijachakachuliwa hivyo ni wazi kila askari kujua maadili ya kijeshi yapo kisheria na askari yeyote anafundishwa namna ya kuishi katika maisha ya utumishi wa jeshi la Polis
No comments:
Post a Comment