Thomas Duncan alietokea Afrika Magharibi zaidi ya siku 18 zilizopita ambapo mchumba wake aitwae Louise Troh waliekua waoane baada ya Duncan kuwasili Marekani, ni mmoja wa watu wa karibu waliolalamikia huduma mbovu na ‘kubaguliwa’ kwa Duncan baada ya kugundulika kuwa mgonjwa wa Ebola hivyo anataka uchunguzi ufanywe.
Anasema Duncan alipotua Texas kwa mara ya kwanza aliambiwa aende nyumbani na wala hakupimwa kama anavyo virusi vya ugonjwa wa Ebola pamoja na kwamba aliwaambia Manesi kwamba ametokea Liberia ambako kuna Ebola.
Reverend Jesse Jackson akiwa na mama mzazi wa Duncan.
Hii picha ni Duncan akiwa na ndugu yake muda mfupi baada ya kuwasili Marekani kwenda kumuoa mchumba wake wa siku nyingi.
Hawa kwenye picha hapa chini ni watu waliobobea kwenye usafishaji na waliitwa kufanya usafi kwenye nyumba aliyokua anakaa Duncan huko Dallas Texas kabla ya kwenda Hospitali ambapo vitu vyake kama mashuka na mataulo vilibaki kwenye nyumba hiyo kwa siku tano baada ya yeye kupelekwa Hospitali.
No comments:
Post a Comment