Ugonjwa wa Ebola imekua ishu kubwa kwenye hizi nchi maarufu duniani ambazo zimejikuta zikiingia kwenye headlines baada ya Wagonjwa kuanza kugundulika ambapo Marekani kuna mmoja aliingia na Ebola kutokea Afrika na mwingine ni huyu Nesi wa Hispania.
Labda unaweza kushangaa ni jinsi gani huyu Nesi amekua akilindwa baada ya kujulikana amepata huo ugonjwa, hiyo picha ya juu sio msafara wa Kiongozi bali ni Polisi walikua wanamsindikiza Nesi huyo kumpeleka Hospitali ya Carlos III.
Hawa
ni Wafanyakazi nje ya hospitali ya La Paz University wakiwa wameungana
pamoja kutoka Waziri wa Afya wa Hispania Ana Mato ajiuzulu baada ya
mgonjwa wa Ebola kugundulika.
Kwenye sentensi nyingine ni kwamba Mwanaume wa Nigeria ambae aliingia Hispania siku kadhaa zilizopita pia alichukuliwa na kuchunguzwa lakini hakukutwa na Ebola, vivyo hivyo kwa Nesi mwingine ambae alikua akifanya kazi na Nesi wa kwanza aliekutwa na Ebola, baada ya kuharisha aliwekwa chini ya uchunguzi lakini ikagundulika hakuwa amepatwa na Ebola
No comments:
Post a Comment