Friday 10 October 2014

LORI LA KAMPUNI YA COCA COLA LILIVYOPATA AJALI LUGALO JIJINI DAR

 Kioo cha lori cha  mbele kikiwa kimepasuka.
 Makreti ya soda yalivyoanguka.
 Baadhi ya kreti za soda zikiwa zimezagaa eneo la ajali.Mmoja wa wahusika akitoka kuzima na kuuchomoa ufunguo wa gari lililopata ajali.
 Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) akilinda usalama eneo hilo.
 Watu wakishuhudia ajali hiyo.
  Chupa zikiwa zimeanguka kwenye mtaro.
Sehemu ya foleni inayosababishwa na gari hilo.

WATU watatu akiwemo dereva wa gari la kampuni ya soda ya Coca Cola walipata michubuko kadhaa katika ajali iliyotokea leo asubuhi maeneo ya Lugalo, jijini Dar es Salaam.
 
Akizungumza na mtandao huu,  mmoja wa mashuhuda amesema chanzo cha ajali hiyo ni baada ya gari ndogo kuingia ghafla mbele ya gari hilo  kubwa lililokuwa limebeba vinywaji na  ndipo gari kubwa likiwa katika kukwepa likajikuta likianguka ubavu

No comments: