Wednesday 5 March 2014

ASHAMBULIA POLISI KWA MAPANGA, WANANCHI WAMKATAKATA NA KUMUUA

Butiama.

Mtu mmoja ameuawa na wananchi kwa kukatwa katwa na mapanga baada ya kuwavamia askari polisi katika kituo cha polisi cha Butiama mkoani Mara.

Kaimu Kamanda wa polisi mkoani Mara Paulo Kasabago amethibitisha kutokea kwa tukio hilo jana saa 9 alasiri ambapo imedaiwa kuwa marehemu huyo alifika katika kituo hicho na kuchomoa panga uliokuwa ndani ya mkoba mgongoni mwake na kuanza kuwashambulia askari polisi walikuokuwepo kituoni hapo.
Kasabago aliwataja askari waliokatwa mapanga kwenye tukio hilo kuwa ni Grantha namba WP.9533 PC aliyekatwa sehemu ya mikononi na mguu wa kulia pamoja na askari mwingine Israel namba F.8901 D/C aliyekatwa kifuani baada ya kutoka ndani ya kituo kuja kutoa msaada kwa Grantha.

Kasabago alisema baada ya askari hao kupiga kelele mtu huyo alianza kukimbia ambapo wananchi waliokuwa jirani walimkimbiza kwa kumshambulia kwa mawe, fimbo na mapanga kilichosababisha kifo chake akiwa anapatiwa matibabu kwenye hospitali ya wilaya ya Butiama.

Katika tukio lingine mwanaume mmoja ameuawa kwa vipigo na kuchomwa moto katika Kijiji cha Kabasa Tarafa ya Serengeti wilayani Bunda baada ya kudaiwa kuiba mbuzi watatu mali ya Saasita Sekule(49).

Alisema wananchi hao baada ya kumuua mtu huyo walichoma nyumba tano moto na kuziteketeza mali ya Mazwanja Lwangumba ambaye alituhumiwa kuwa mwanae Butiku Mazwanja alishirikiana na marehemu katika wizi wa mbuzi hao.

Kasabago alisema katika tukio hilo watu wawili ambao ni Saasita Sekule na na Alfred Mtogwa wana shikiliwa jeshi la polisi kwa kutuhumiwa kuhusika katika tykio hilo.

No comments: