Rapper wa kimarekani Jayceon Terrell
Taylor aka The Game ambaye kwa sasa yupo barani ulaya kwa ajili ya Tour
yake aliyoipa jina la BloodMoney, jana alikuwa jijini Manchester na
alitumia nafasi yake kuwepo kwenye jiji hilo kwa kuonyesha mapenzi yake
kwa klabu ya Manchester United. The Game alienda kununua jezi ya klabu
hiyo na kuitinga kisha kupiga picha na kuitundika katika akaunti yake ya
Instagram.
Monday, 3 March 2014
KINANA AFANYA KUFURU KIBAHA

Pikipiki
tisa na Baiskeli themanini na sita zilizotolewa na Mbunge wa Kibaha
Kijijini Ndugu Hamoud A. Jumaa kwa Makatibu kata na viongozi wa mashina
wa Kibaha Kijijini.

Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Pwani Ndugu Mwishehe Shaban Mlawa akimuambia Katibu Mkuu
wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana waanze safari kwa pikipiki mpya
zilizotolewa na Mbunge wa Kibaha Kijijini Ndugu Hamoud A.Jumaa kwa
Makatibu kata na wajumbe wa mashina 86 kwenye viwanja vya shule ya
msingi Mtongani.

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Kibaha
Kijijini kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Mtongani ambapo aliwaambia
moja ya kazi kubwa ya viongozi wa CCM ni kutekeleza yale walioahidi kwa
wananchi.

Wanachama
wapya wakila kiapo baada ya kukabidhiwa kadi za uanachama wa CCM kwenye
mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi
Mtongani ambapo mgeni wa Heshima alikuwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana.

Hamis
Rashidi akirudisha kadi na makabrasha ya CUF kwa Katibu Mkuu wa CCM
Ndugu Abdulrahman Kinana na kujiunga na CCM kwenye mkutano wa hadhara
uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya Msingi Mtongani Kibaha Kijijini.

Mbunge
wa Kibaha Kijijini Ndugu Hamoud A. Jumaa akihutubia wakazi wa Kibaha
Kijijini na kuwaambia mafanikio waliyoyapata ikiwa pamoja na kufungua
ofisi ya kisasa ya Mbunge kugawa pikipiki tisa na baiskeli themanini na
sita kwa makatibu kata na mabalozi wa shina.

Isha
Mashauzi akitumbuiza wakazi wa Kibaha Kijijini wakati wa mkutano wa
hadhara ambao Katibu Mkuu wa CCM alikuwa mgeni wa Heshima.

Viongozi
wa CCM wilaya ya Kibaha wakicheza rusha roho wakati wa mkutano wa
hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Mtongani.

Suleiman
Jabir maarufu kama Msagasumu akiburudisha umati uliofurika kwenye
mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi
Mtongani Kibaha Kijijini
MUFTI WA TANZANIA AENDA INDIA KWA MATIBABU
![]() |
| Sheikh Issa Bin Shaaban Simba. |
Mufti wa Tanzania, Sheikh Issa Bin Shaaban Simba ameondoka nchini kuelekea India kwa ajili ya matibabu.
Aliongozana
na ujumbe wa watu wawili, akiwemo Katibu Mkuu wa Baraza la WaislamU
Tanzania(BAKWATA), Suleiman Lolila na Diwani wa Kata ya Kwadelo wilayani
Kondoa, Omari Kaliati.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyomfikia mwandishi na kuthibitishwa na Naibu
Katibu Mkuu wa Bakwata anayeshughulikia Utawala, Yusufu Yasini, Sheikh
Simba aliondoka saa 10 jioni kwa kutumia ndege ya Shirika la Oman Air.
Mufti
alifika uwanjani hapo na kuingia kupitia eneo la wageni mashuhuri (VIP)
huku akisindikizwa na msafara wa pikipiki ya polisi.
Naibu
Katibu Mkuu wa Bakwata anayeshughulikia Dini, Mohammed Khamis aliahidi
kutoa taarifa zaidi kwa mwandishi, kuhusiana na safari hiyo.
Mara
baada ya kutapa taarifa za safari hiyo juzi, mwandishi alimtafuta Naibu
Katibu Mkuu Utawala wa Bakwata, aliyekiri Mufti kusafiri.
"Sipo
katika nafasi nzuri ya kuzungumzia suala hilo kwa kuwa nipo barabarani,
naendesha gari, nitafute kesho (jana) nitaweza kukupa taarifa vizuri,"
alisema Yusufu.
Alipotafutwa tena jana kupitia simu yake ya mkononi, hakuweza kupatikana baada ya simu hiyo kuwa imezimwa.
Juhudi
za kuwatafuta viongozi hao zinaendelea kufanywa na mwandishi ili kupata
taarifa zaidi ya safari ya kiongozi huyo mkuu wa Waislam nchin
MWANDISHI WA HABARI FEKI ALIVYONASWA LIVE AKITAKA KUMUIBIA MH. SHABIBY HUKO DODOMA...!
![]() | ||
| Mwandishi wa habari feki akiwa mikononi mwa vyombo vya dola baada ya kushtukiwa: |
![]() | |
| Mhariri huyu feki alitumia janja ya kumtumia ujumbe mfupi wa maneno mh na kujitambulisha kuwa yeye ni mhariri mkuu wa gazeti la Dira,. |
![]() |
| lakini zoezi hilo lilikuwa ngumu kufanikiwa kwa mhariri huyo feki baada ya mheshimiwa kumshtukia na pia alikuwa anamfahamu vizuri mhariri mkuu wa gazeti hilo, Mhariri feki huyo baada ya kuona ameshtukiwa aliamua kukiri na kuomba msamaha na kudai kuwa ni ugumu wa maisha ndio umemsababishia hali hiyo, |
![]() |
| Kutokana hali na huruma Ya mheshimiwa shabiby aliyokuwa nayo aliamua kumsamehe na kumpatia fedha zaidi ya laki moja, Ila mhariri feki huyo anashikiwa na jeshi la polisi kwa kuadhalilisha taaluma hiyo na pia kulichafua gazeti hilo la Dira, Pia Mh Shabiby aliendelea kututonya kwamba kuna waandishi wengi ambao wanatumia janja hiyo ili kujipatia fedha na pia alituambia kwamba alishawahi kumshtukia mwandishi wa gazeti la Nipashe na baada ya kuona ameshtukiwa anaambiwa alitoka ndiki mithili ya swala na kuacha vumbi endeo hilo |
![]() |
| Mh Shabiby |
![]() |
![]() |
![]() |
| Jeshi la polisi likifanya kazi yake |
![]() |
| Mharir feki akiwa kajificha kwa kuziba kichwa ili asipigwe picha |
Sunday, 2 March 2014
Watoa chanjo washambuliwa Pakistan
Bomu lililokuwa limetegwa kando ya barabara lilifyatuka wakati msafara uliokuwa ukilindwa na polisi ukipita katika kijiji kimoja katika jimbo la Khyber Pakhtunkhwa karibu na mpaka na Afghanistan.
Shambulio hilo ni jipya kabisa miongoni mwa mashambulio yanayowalenga watoa huduma ya chanjo ya polio nchini Pakistan.
Hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulio hilo, lakini kundi la Taliban limekuwa likipinga mipango ya utoaji wa chanjo ya polio, mipango ambayo wanaichukulia kama mbinu ya ujasusi wa kimataifa.
Milipuko hiyo imeripotiwa kufuatiwa na mapigano makali ya bunduki kati ya majeshi ya usalama na wanamgambo.
Maafisa wamethibitisha kuwa watu waliojeruhiwa katika shambulio hilo walikimbizwa katika hospitali ya karibu. Baadhi ya waliojeruhiwa wanasemekana kuwa katika hali mbaya.
Pakistan imeshuhudia vitendo vya ghasia kufanyiwa wafanyakazi wa afya, ambao wanamgambo wanawatuhumu pia kuwa sehemu ya njama za nchi za magharibi kupunguza idadi ya Waislam.
Zaidi ya watu 40 wanaohusishwa na mpango wa chanjo wameuawa nchini Pakistan tangu Desemba 2012.
Mwezi uliopita, watu wenye silaha wasiofahamika waliwaua kwa kuwapiga risasi wafanyakazi watatu wa kutoa chanjo ya polio, katika mji wa Karachi ulioko kusini mwa Pakistan, siku moja baada ya serikali kuanza zoezi la chanjo kwa nchi nzima.
Pakistan ni moja kati ya nchi tatu zinazokabiliwa na milipuko ya ugonjwa wa polio, duniani zikiwemo Nigeria na Afghanistan.
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani, WHO, Pakistan ilikuwa na wagonjwa 91 wa polio mwaka jana, wakiwa wameongezeka kutoka idadi ya wagonjwa 58 mwaka 2012.
ACT YASHUSHA BENDERA ZA CHADEMA HUKO KIGOMA,WANACHAMA 3500 WA CHADEMA WAJIUNGA ACT
Chama cha Alliance For Change and Transparency Mkoa wa Kigoma,kimeshusha Bendera ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA tawi la Ujiji stendi ya zamani na kupandisha bendera ya (ACT) wakati wa uzinduzi rasmi wa matawi sita katika manispaa ya kigoma ujiji.
Akizungumza na wananchi wa eneo hilo, Katibu wa ACT Mkoa Athuman Kabogo alidai lengo la kushusha bendera hiyo ni hatua ya kukataa kugeuzwa kuwa vibaraka wa watu wengine kwa kukosa haki ya kuhoji na kuwania nyadhifa za chama hicho na
hivyo kuanzisha ACT kama chama cha wanyonge kinachoweza kuwasikiliza na kutoa haki kwa kila mmoja
Kabogo aliwataka wanachama wahitaji, wachukue kadi za ACT ili chama kipate usajili kamili kwa mujibu wa sheria,kanuni na taratibu husika pamoja na kutoa michango endelevu ,ikiwa ni jitihada za makusudi kuhakikisha chama kinasonga mbele
kwa maslahi ya Taifa.
“Wananchi nyie ni chachu ya chama kuwepo kwenye mchakato wa uchaguzi mdogo wa wenyeviti wa serikali za mitaa kwa kukiamini na kukipatia ridhaa kiweze kuleta
mabadiliko ya kimaendeleo” alisema Juma Ramadhan aliyekuwa katibu kampeni wa CUF kigoma.
Kwa upande wa Katibu ACT Kanda Magharibi Wiston Moga alisema, lengo la chama ni kuleta mabadiliko kwenye ulingo wa siasa,ambapo wao wamedhamiria kutetea maslahi ya umma kwa lengo la kuondoa mfumo wa maslahi binafsi ambayo ni chachu ya vyama vya siasa kushindwa kuleta mabadiliko chanya kwa wananchi.
Katika ziara hiyo ya uzinduzi wa matawi ya chama husika,ACT kimefanikiwa kufungua matawi kwenye kata sita kati ya kata 19 zilizopo katika manispaa ya kigoma ujiji,huku baadhi ya viongozi kutoka UPD,CHADEMA na CUF wakijiunga na chama hicho
kwa kudai wanahitaji chama chenye uchungu na kukabiliana na changamoto za wanyonge.
Hata hivyo wanachama 3500 wa chama cha Democrasia na Maendeleo Chadema katika tawi la Ujiji mkoani Kigoma wamehamia chama kipya cha Alliance For Change and Transparency (ACT).
Na Magreth Magosso, Kigoma
KAWAMBWA AKERWA DARAJA LA TANO KUITWA SIFURI
Dk. Shukuru Kawambwa, aliyasema hayo jana mjini Dodoma alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
Dodoma.
Waziri wa Elimu na Mafunzo yaUfundi, Dk Shukuru Kawambwa ameelezea
kukerwa na daraja la tano katika muundo mpya wa kupanga matokeo, kuitwa
sifuri.
Dk. Shukuru Kawambwa, aliyasema hayo jana mjini Dodoma alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
Alivishutumu
vyombo vya habari kwa kuchanganya alama na madaraja yaliyopo katika
muundo mpya wa kupanga matokeo ya mitihani nchini.
Alisema
kwa muundo mpya, daraja sifuri ni kati ya pointi 48 na 49 ambayo
inapatikana baada ya mtahiniwa kupata alama F kwa masomo yote saba.
"Ndugu
zangu waandishi wa habari, kitu ambacho hamkufanya haki kwa
Watanzaniasafari hii, ni ile kuliita daraja la tano kuwa ni sifuri
mkalazimisha na mimi kumwagiza Katibu Mkuu abadilishe na kuita daraja
sifuri," alisema na kuongeza:
"Unakuaje
na daraja la kwanza, la pili, la tatu, la nne lakini unapofika la tano
unaita sifuri katika namna ambavyo waandishi wa habari walipenda."
Dk
Kawambwa alisema vyombo vya habari vimekuwa vikipenda taswira ya nchi
ionekane kuwa ni kufeli. "Lakini ninachosema ni kwamba, pointi ni zile
zile tulichoondoa ni daraja la tano."
TAARIFA KUTOKA IKULU

Katika
siku za karibuni, kumekuwepo na habari nyingi, baadhi zenye kuchanganya
umma na nyingine hata zikidai kuwa baadhi ya wafanyakazi nchini
wanapanga kuandamana endapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete atakubaliana na maombi ya nyongeza ya
posho ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba .
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu (DPC), inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu habari hizo kama ifuatavyo:
(a) Kwamba Mhe. Rais hajapata kupokea maombi yoyote kutoka kwa Uongozi wa Bunge ya kumwomba aridhie kuongezwa kwa posho ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kutoka kiwango cha sasa cha sh. 300,000 (laki tatu)kwa siku hadi kufikia sh. 500,000 (laki tano) ama sh. 700,000 (laki saba) kama ambavyo imekuwa ikivumishwa katika baadhi ya vyombo vya habari.
(b) Na kwamba kwa sababu Mhe. Rais hajapata kupokea maombi ya nyongeza ya posho hiyo, hakuna ongezeko lolote la posho ambalo Mhe. Rais ameliidhinisha.
(c) Kwamba alichopokea Mhe. Rais ni maombi ya Uongozi wa Bunge wa kuomba Mhe. Rais aridhie kufanyika marekebisho katika kiwango cha malipo ya siku kwa Wajumbe hao cha sh. 300,000 (laki tatu) ili posho ya kikao iwe posho ya kujikimu na posho ya kujikimu iwe ndio posho ya kikao.
(d) Kwamba Mhe. Rais amelikubali ombi hilo la Uongozi wa Bunge la kufanyika kwa marekebisho katika mpangilio huo wa posho lakini kiwango cha malipo ya kila siku ya Wajumbe hao kibakie kile kile cha sh. 300,000 (laki tatu) kwa siku.
(e) Kwamba tayari Mhe. Rais amekwishaujulisha Uongozi wa Bunge kuhusu uamuzi wake huo wa kukubali yafanyike marekebisho lakini kiwango kibakie kile kile cha sh. 300,000 (laki tatu) kwa siku.
(f) Hivyo, Mhe. Rais hajaongeza kiwango cha malipo ya Wajumbe hao kwa sababu hakupata kuombwa wakati wowote kuongeza kiasi hicho.
Ni matarajio ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, kuwa maelezo haya ya ufafanuzi yatasaidia kufunga mjadala ambalo msingi wake kwa kweli umekuwa haupo.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
01 Machi, 2014
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu (DPC), inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu habari hizo kama ifuatavyo:
(a) Kwamba Mhe. Rais hajapata kupokea maombi yoyote kutoka kwa Uongozi wa Bunge ya kumwomba aridhie kuongezwa kwa posho ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kutoka kiwango cha sasa cha sh. 300,000 (laki tatu)kwa siku hadi kufikia sh. 500,000 (laki tano) ama sh. 700,000 (laki saba) kama ambavyo imekuwa ikivumishwa katika baadhi ya vyombo vya habari.
(b) Na kwamba kwa sababu Mhe. Rais hajapata kupokea maombi ya nyongeza ya posho hiyo, hakuna ongezeko lolote la posho ambalo Mhe. Rais ameliidhinisha.
(c) Kwamba alichopokea Mhe. Rais ni maombi ya Uongozi wa Bunge wa kuomba Mhe. Rais aridhie kufanyika marekebisho katika kiwango cha malipo ya siku kwa Wajumbe hao cha sh. 300,000 (laki tatu) ili posho ya kikao iwe posho ya kujikimu na posho ya kujikimu iwe ndio posho ya kikao.
(d) Kwamba Mhe. Rais amelikubali ombi hilo la Uongozi wa Bunge la kufanyika kwa marekebisho katika mpangilio huo wa posho lakini kiwango cha malipo ya kila siku ya Wajumbe hao kibakie kile kile cha sh. 300,000 (laki tatu) kwa siku.
(e) Kwamba tayari Mhe. Rais amekwishaujulisha Uongozi wa Bunge kuhusu uamuzi wake huo wa kukubali yafanyike marekebisho lakini kiwango kibakie kile kile cha sh. 300,000 (laki tatu) kwa siku.
(f) Hivyo, Mhe. Rais hajaongeza kiwango cha malipo ya Wajumbe hao kwa sababu hakupata kuombwa wakati wowote kuongeza kiasi hicho.
Ni matarajio ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, kuwa maelezo haya ya ufafanuzi yatasaidia kufunga mjadala ambalo msingi wake kwa kweli umekuwa haupo.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
01 Machi, 2014
Subscribe to:
Comments (Atom)















