Saturday, 13 December 2014

Bensouda kusitisha uchunguzi Darfur

 

Moreno Ocampo alyekuwa kiongozi wa mashtaka wa ICC na kiongozi wa sasa wa mahakama hiyo Fatou bensoud. 
Mwendesha mashtaka mkuu kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita Fatou Bensouda amesema kuwa atasitisha uchunguzi kuhusu uhalifu wa kivita ulioendeshwa katika eneo la Darfur nchini Sudan kutokana na ukosefu wa usaidizi kutoka kwa baraza la usalama la umoja wa mataifa.
Kwenye taarifa yake kwa baraza hilo mwendesha mashtaka huyo amesema kuwa wanawake na wasichana wanaendelea kuathirika zaidi katika jimbo hilo.

 

Rais wa Sudan Omar El Bashir anayetafutwa na mahakama ya ICC kwa kuhusishwa na uhalifu dhidi ya binaadamu katika eneo la Darfur.
 
Amesema kuwa kutokuwepo kwa hatua zozote kutoka kwa baraza la umoja wa mataifa kumechangia kuendelea kwa uhalifu na sasa amelazimika kutumia raslimali za mahakama hiyo kwa masuala mengine.
Mwaka 2009 mahakama ya ICC ilimhusisha rais wa Sudan Omar al-Bashir na uhalifu wa kivita kwenye jimbo la Darfur lakini hadi sasa hajakamatwa wala hata mmoja wa washirika wake.

No comments: