Timu
ya Simba imeibuka na ushindi baada ya kuichapa timu ya Yanga 2-0 huku
timu ya Yanga wakiambulia kuondoka na maumivu ya kushindwa kufurukuta
kwa bao hata moja.
Wafungaji wa magoli kutoka timu ya Simba ni Awadh Juma na Elias Maguri ambapo mabao yote yamefungwa katika kipindi cha kwanza.
Kwa mara ya pili tena timu ya SIMBA wamefanikiwa kuibuka na ushindi
wa Nani Mtani Jembe baada ya kutwaa ubingwa huo mwaka jana walipoichapa
Yanga bao 3 -1.
Kwa upande wa zawadi Simba wamefanikiwa kutwaa milioni 92 huku Yanga wakiondoka milioni 7.
Wachezaji wa timu ya Simba wakishangilia bao la pili
lililofungwa na Elias Maguli katika dakika ya 40 ya kipindi cha kwanza.
Mabao yote ya Simba yamefungwa katika kipindi cha kwanza huku bao la
kwanza likifungwa na Awadh Juma katika dakika ya 30.
Mashabiki wa Simba wakishangilia moja ya mabao yaliyofungwa na timu yao.
Andreu Coutihno, akimiliki mpira katikati ya mabeki wa Simba…
Mchezaji mpya wa Yanga, kutoka nchini Liberia, Kpah Sherman.
akisomba kijiji cha mabeki wa Simba…. Hadi mpira unaisha jumla ya
mashabiki wasiopungua wanne wa Yanga walikuwa wameshazimia uwanjani.
Mashabiki wa Simba waliojaza kwenye dimba la uwanja wa taifa
Safe driving is a priority so make sure that you follow these tips if you need to make phone calls whilst driving.
Keep your phone on Voicemail when driving.
If you really must make or receive calls, always use a hands-free kit.
Make sure you inform the person you are speaking to that you are driving so they understand that you need to concentrate.
If possible tell the person that you will call back when you have parked safely.
Avoid long, complex or emotional conversations.
If you have a speed dial function on your phone, use this to enter
frequently-called numbers. One touch dialing is much safer than dialing
manually.
Do not take notes or look up phone numbers while driving.
Don’t accept or make calls if traffic and weather conditions would make it unsafe to do so.
Safety Tips
Get to know your cell phone and its features, such as speed dial and redial. Carefully
read your instruction manual and learn to take advantage of valuable
features most cell phones offer, including automatic redial and memory.
Also, work to memorize the phone keypad so you can use the speed dial
function without taking your attention off the road.
When available, use a hands-free device. A
number of hands-free cell phone accessories are readily available today.
Whether you choose an installed mounted device for your cell phone or a
speaker phone accessory, take advantage of these devices if available
to you.
Position your cell phone within easy reach. Place
your cell phone within easy reach and where you can grab it without
taking your eyes off of the road. If you receive a call at an
inconvenient time, if possible, let your voice mail answer it for you.
Suspend conversations during hazardous driving conditions or situations. Let
the person you are speaking with know you are driving. If necessary,
suspend the call in heavy traffic or hazardous weather conditions. Rain,
sleet, snow and ice can be hazardous, but heavy traffic can be just as
dangerous. As a driver, your first responsibility is to pay attention to
the road.
Do not take notes or look up phone numbers while driving. If
you are reading an address book or business card, or writing a "to do"
list while driving a car, you are not watching where you are going. It's
common sense. Don't get caught in a dangerous situation because you're
reading or writing and not paying attention to the road or nearby
vehicles.
Dial sensibly and assess the traffic. If possible, place calls when you are not moving or before pulling into traffic. Try
to plan your calls before you begin your trip, or attempt to coincide
your calls with times you may be stopped, such as at a stop sign, red
light or in a parking space. But, if you need to dial while driving,
follow this simple tip: Dial only a few numbers, check the road and your
mirrors, then continue dialing.
Do not engage in stressful or emotional conversations that may be distracting. Stressful
or emotional conversations and driving do not mix — they are
distracting and even dangerous when you're behind the wheel of a car.
Make people you are talking with aware you are driving and, if
necessary, suspend conversations which have the potential to divert your
attention from the road.
Use your cell phone to call for help. Your
cell phone is one of the greatest tools you can own to protect yourself
and your family in dangerous situations — with your phone at your side,
help is only three numbers away. Dial 911 or another local emergency
number in emergencies such as a fire, traffic accident, road hazard or
medical emergency. Remember, an emergency call is a free call on your
cell phone!
Use your cell phone to help others in emergencies. Your
cell phone provides the opportunity to be a "Good Samaritan" in your
community. If you see a car accident, crime in progress or other serious
emergency where lives are in danger, call 911 or another local
emergency number, as you would want others to do for you.
Call roadside assistance or a special cell non-emergency assistance number when necessary. Certain
situations you encounter while driving may require attention, but are
not urgent enough to merit a call for emergency services. Even so, you
still can use your cell phone to lend a hand. If you see a disabled
vehicle posing no serious hazard, a broken traffic signal, a minor
traffic accident where no one appears injured or a vehicle you know is
stolen, call roadside assistance or another special non-emergency cell
number
Mayweather akipigana.Bondia huyo amesema kuwa
yuko tayari kutetea taji lkake dhidi ya Manny Pacquiao mwaka ujao.
Bondia Floyd Mayweather ametaja tarehe 2 mwezi May mwaka 2015 kama siku ya pigano kati yake na Manny Pacquiao .
Kulingana
na gazeti la Daily mail nchini Uingereza ,uvumi kwamba pigano hilo
ambalo litakuwa la kiwango kikubwa cha malipo kuwahi kutokea katika
historia ya ndondi ulianza pale Pacquiao alipoonyesha mchezo mzuri kati
yake na Chris Algieri mjini Macau wiki mbili zilizopita.
Na sasa
Maywheather kupitia kampuni yake moja ya mauzo amesema kuwa yuko tayari
kupambana na Pacman katika pigano lake linalokuja.
Bondia Manny Pacquiao Kushoto akimchapa Tim Bradley katika mojwapo ya mapigano yao.
Bondia huyo ambaye ndiye
mwanamichezo tajiri duniani amesema kuwa mashabiki wa ndondi wamesubiri
sana pigano hilo na sasa yuko tayari.
''Kizuizi kikubwa cha pigano
hilo ni promota wa Pacquiao Bob Arum ,lakini najua kwamba sisi sote
tunalihitaji pigano hili'',alisema Mayweather.. Kwa hivyo ni wakati
lifanyike.
Mayweather alikiri kwa mara ya kwanza majadiliano
yanaendelea kwa siri na kuongeza kwamba hamuogopi mtu yeyote.''Miaka
iliopita tulikuwa na tatizo la kupimwa mikojo na damu,swala ambalo
Pacman amekuwa akilipinga''.aliongezea Mayweather.
Bondia Mayweather baada ya kushinda katika baadhi ya mapigano yake.
Hatahivyo upande wa Mayweather ni vile kitita cha pigano hilo kitakavyogawanywa.
Inakadiriwa kuwa pigano hilo litagharimu dola millioni 300.
Upande
wa Pacman tayari umekubali fedha hizo kugawanywa kwa 60-40 huku
Mayweather akichukua kitita kikubwa,ijapokuwa kuna madai kwamba
Mayweather huenda akadai asilimia kubwa zaidi iwapo makubaliano
yataafikiwa
Aliyekuwa naibu mkufunzi wa kilabu ya Aston Villa Roy Keane
Naibu
Kocha wa Kilabu ya Aston Villa Roy Keane na mshambuliaji Gabriel
Agbonlahor nusra wapigane wakati wa mazoezi katika majibizano ya manane
yaliomlazimu kocha huyo kuondoka katika kilabu hiyo.
Kulingana na
gazeti la Daily mail nchini Uingereza,Roy Keane mara kwa mara alihusika
katika mgogoro na wachezaji wa muhimu wa kilabu hiyo miezi sita tu baada
ya kujiunga na kilabu hiyo.
Inadaiwa kuwa hali ya mazingira wakati wa mazoezi ilibadilika mara kwa mara wakati wa kuwasili kwa Roy Keane.
Kulikuwa
na hali ya wasiwasi wakati kocha huyo alipozozana na nahodha wa kilabu
hiyo Agbonlahor mbele ya wachezaji wenzake wakati wa mazoezi kabla ya
naibu huyo kuondoka katika timu hiyo.
Nahodha wa kilabu ya Aston Villa Agbonlahor akielekea kufunga bao
Inadaiwa kuwa Agbonlahor alikuwa akijadiliana na mkufunzi wa timu hiyo Lambert wakati Keane alipoingilia kati.
Lakini Agbonlahor alikataa kunyamaza na badala yake akamwambia Keane kwamba anazungumza na kocha.
Wawili hao baadaye walihusika katika majibizano na ilibidi watawanywe.
Uhasama
huo uliendelea kati ya wawili hao ndiposa Lambert akafanya kikao na Roy
Keane wakati ilipoamuliwa kwamba nahodha huyo wa kitambo wa timu ya
Manchester United ataondoka katika kilabu hiyo
Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu
mazingira ambao ulikuwa umalizike mapema, unaendelea nchini Peru kwa
siku ya 13 huku wajumbe wakijaribu kufikia makubaliano kuhusu namna ya
kupambana na kuzidi kwa joto duniani.
Wamekwama katika hoja kuhusu ahadi ambazo zinaweza kutolewa na nchi zilizoendelea na zinazoendelea.
Mataifa
yanayoharibu mazingira zaidi, kama Marekani na ya Umoja wa Ulaya,
yanataka kutangaza mwaka ujao yatapunguza gesi inayozidisha joto kwa
kiasi gani.
Lakini piya yanataka nchi nyengine zaidi zitoe ahadi kama hiyo.
Nchi
kuu zinazoendelea, pamoja na India na Uchina, zinapinga hayo huku nchi
maskini zaidi zinataka msaada zaidi wa fedha ili kupambana na athari za
mabadiliko ya hali ya hewa.
Mbunge Zito Kabwe mwenyekiti wa kamati iliyowasilisha ripoti kuhusu sakata ya Escrow
Serikali
ya Tanzania iko hatarini kukosa dola za Marekani milioni mia saba sawa
na trilioni 1.1 kwa fedha za Tanzania kwa ajili ya mradi wa pili wa
mfuko wa changamoto za Milenia (MCC) kutokana na kushamiri kwa vitendo
vya rushwa nchini humo.
Marekani imebainisha kuwa mkataba wa pili
wa miradi inayofadhiliwa na shirika lake la Changamoto za Milenia (MCC)
utategemea hatua zitakazochukuliwa na serikali ya Tanzania dhidi ya
wahusika wa kashfa hiyo.
Haya yanajiri wakati Rais Jakaya Kikwete
akisubiriwa kutoa maamuzi ya mapendekezo yaliyofikiwa na Bunge kuhusiana
na sakata la uchotwaji fedha zaidi ya Sh. bilioni 300 kutoka kaunti ya
Tegeta Escrow wiki ijayo.
Katika tamko hilo kwa umma ambalo
limewekwa kwenye tovuti ya MCC, bodi ilieleza kutambua umuhimu wa
kusubiri na kuona utekelezaji kamilifu wa tamko lililotolewa na Ikulu ya
Tanzania Desemba 9, mwaka huu kwamba itachukua hatua za haraka na kutoa
maamuzi dhahiri na thabiti kuhusu maazimio ya Bunge juu la suala la
IPTL.
Taarifa iliyotolewa na Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania
ilieleza kuwa wakurugenzi wa MCC waliokutana katika mkutano wao
uliofanyika Desemba 10, mwaka huu wamesikitishwa na hali ya rushwa
nchini Tanzania.
Bunge la Tanzania kikaoni
Uamuzi huo wa Marekani ambayo
inafadhili miradi mingi ya mabilioni ya fedha ni mtihani wa pili kwa
Rais Kikwete baada ya ule wa maazimio ya Bunge yaliyotaka viongozi
wakiwamo mawaziri waliotajwa katika kashfa hiyo kuwajibishwa.
Wanaotakiwa
kuwajibishwa na Rais Kikwete ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa,
Sospeter Muhongo na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
Profesa Anna Tibaijuka.
Wengine ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakimu Maswi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema.
Novemba
mwaka huu, Serikali ya Marekani kwa kupitia MCC, ilikubali kutoa ruzuku
ya hadi Dola za Kimarekani milioni 9.78 kwa ajili ya maandalizi ya
miradi ya uwekezaji yenye matokeo makubwa katika sekta ya nishati
nchini.
Tanzania ilikuwa mojawapo ya nchi kumi zilizojadiliwa na
Bodi ya MCC iliyokutana kuangalia kama nchi hizo zimekidhi vigezo vya
kuendelea na mchakato wa kuandaa mikataba mipya.
Wakati wa mkutano
wa 16 na 17 wa Bunge, Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila
(NCCR-Mageuzi), alidokeza kusudio la Marekani kukataa kutoa fedha kwa
ajili ya miradi ya MCC, lakini Waziri wa Nishati na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo alikanusha taarifa hizo.
Juhudi za BBC kumtafuta
Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Mark Childress,aweze kuzungumzia juu
ya ripoti hiyo ziligonga mwamba kutokana na sababu za kiprotokali.
Moreno Ocampo alyekuwa kiongozi wa mashtaka wa ICC na kiongozi wa sasa wa mahakama hiyo Fatou bensoud.
Mwendesha
mashtaka mkuu kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita Fatou
Bensouda amesema kuwa atasitisha uchunguzi kuhusu uhalifu wa kivita
ulioendeshwa katika eneo la Darfur nchini Sudan kutokana na ukosefu wa
usaidizi kutoka kwa baraza la usalama la umoja wa mataifa.
Kwenye
taarifa yake kwa baraza hilo mwendesha mashtaka huyo amesema kuwa
wanawake na wasichana wanaendelea kuathirika zaidi katika jimbo hilo.
Rais wa Sudan Omar El Bashir anayetafutwa na
mahakama ya ICC kwa kuhusishwa na uhalifu dhidi ya binaadamu katika eneo
la Darfur.
Amesema kuwa kutokuwepo kwa
hatua zozote kutoka kwa baraza la umoja wa mataifa kumechangia kuendelea
kwa uhalifu na sasa amelazimika kutumia raslimali za mahakama hiyo kwa
masuala mengine.
Mwaka 2009 mahakama ya ICC ilimhusisha rais wa
Sudan Omar al-Bashir na uhalifu wa kivita kwenye jimbo la Darfur lakini
hadi sasa hajakamatwa wala hata mmoja wa washirika wake.